Inauma sana jamani...

mysteryman

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
979
176
Kwa kweli inauma sana kuona watanzania wenzetu wengi ktk maeneo ya vijijina wanaishi kwa kutokuwepo kwa kesho yao...ktk pita pita yangu baadhi ya maeneo ya vijijini ya mkoa wa dodoma,singida na tabora nimekutana haya yakusikitisha sana...ndugu zangu wakati wengine wakichezea maji...kule ni majonzi....kwanza kisima ni kimoja tena kikiendea kukauka kipindi hiki ndoo ya lita kumi moja kujaa ni jama lisaa hivi na kusubiri maji yajae tena lisaa tena ina mana kwa wastani kila baada ya masaa mawili ndio unapata ndoo ya lita kumi moja kijiji kina watu zaidi ya 400... Inamana kwa siku ni kama ndoo 8 au 9 kwa hiyo inabidi wagawand hayo maji japo jagi moja moja kwa familia wapate japo kupika...yani hayo maji yatakayo fulia nguo ndo hayo hayo yataosha vyombo vichafu na kuoga hayohayo(wanasema kuoga ni nadra sana labda kipindi cha masika) yani maji mpaka yawe hayana kazi yale yakumwaga huwezi kuya tizama mara mbili....na hicho kisima unakuta kipo kama km5 hivi kwa kweli nilitokwa na machozi watu pale walipokuja kugombea maji yangu ya kilimanjaro ya chupa huku wengine wakishangaa yalivyokuwa meupe na masafi kwani hayo yakwao ni jama maji yaliyoosha mchele yenye mchanganyiko na ukijani hivi......roho inaniuma sana njihisi mwenye hatia sana kila nikifikiria ile hali kule lakini ni sehemu nyingi tu kuna watanzania wanaishi ktk hali hiyo....kwa kweli sikua na cha kuwapa zaidi ya yale maji yangu ya kilimanjaro na kipande cha mkate nilichokua nacho....sikuweza hata kuwapa simu namba kwani hakuna hata mawasiliano pale......kama wewe unapta mlo wakn wa siku na maji hata kwa kununua dumu sh1000 shukuru sana kwani jtna watu hawana uhakika hata na maji yakunywa tu tena japo nusu glass tu tena ni mtanzania.... nawasilisha kwa machungu na masikitito makubwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom