Inatia uchungu!


N

nkisumuno

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Messages
208
Likes
2
Points
35
N

nkisumuno

JF-Expert Member
Joined May 22, 2012
208 2 35
Inatia uchungu sana kuona na kusikia yanayotokea Tanzania, kwa maana ya mauaji ambayo yanafanyika wakati vyombo vya kulinda usalama wa wananchi vikibaki kujiumauma tu. Ebu tukumbushane vifo vilivyotokea Arusha kwenye maandamano ya Chadema, Iringa Mwangosi aliuawa kikatili na polisi lakini aliyetoa amri Kamhanda kapandishwa cheo,japo mwanzo walibisha kama wanavyobisha kuhusiana na tukio la juzi Mbowe anaposema polisi walihusika.

Baada ya picha kuwekwa kwenye mtandao wakagwaya je huo si uonevu. Tukumbuke issue ya Mwakyembe na watetea haki na kusema kweli.

Inauma na kutia uchungu kusikia watanzania wenzetu wakiendelea kushabikia na kufurahia unyama huu kwa kukejeli eti CHADEMA walirusha bomu wenyewe Hiv Tanzania tunaipeleka wapi? Wanalaani na kukemea lakini matokeo ya chunguzi zote ni usanii mtupu, kumbuka tume iliundwa kuhusiana na swala la Mwangosi japo watu walisema hakuna haja ya kuunda tume maana wauaji wapo wazi, Vp tume ya kuchunguza kuteswa kwa Ulimboka? Kibanda, bomu la kanisani Arusha na matukio mengi.

Inauma na kutia uchungu kuona damu zisizo na hatia zikimwagwa huku baadhi ya watu wakitajirishana kwa kupewa kazi za uchunguzi, ebu ona damu za watoto wasio na hatia, jamani bado kuna watu wanaleta ushabiki katika matukio haya. yule mama alikufa angekuwa ndugu yako, yule mtoto angekuwa mtoto wako.

Inauma na kutia uchungu kuona waziri mwenye dhamana akiendelea kukalia kiti kwa jeuri tu, IGP anatoa namba za simu baadala ya kujiuzuru mara ngapi jeshi la polisi linatuhumiwa lakini yeye amejifanya kichwa ngumu kwani kujiuzuru anaona ninin.

Inauma na kutia uchungu kuona mawaziri na viongozi wa CCM wakiendelea kukebehi CHADEMA wakati matendo mengi yamefanyika kwa uwazi katika harakati za uchaguzi huu wa madiwani, ona Nasari kalazwa kapigwa na wana CCM, Mufindi watu wa CHADEMA wamelazwa, Serengeti wanachadema wametekwa, kilolo wanachadema wamekatwa mapanga.

Inasikitisha kuona polisi wanavyotumika vibaya na kuua ndugu zao, kwa kuwa tu wanasilaha, utabisha nini mbona issue ya Mwangosi Mtu kapandishwa cheo, nguvu zinazotumika ni kubwa. Naomba Mungu tusaidie watanzania kuwaadhibu wote wanoaofanya unyama huu,wanaowatuma na hata wanaoshangilia na kushabikia wakati uhai wa binadamu unathamani kubwa. Naomba EE MUNGU MWENYEZI angalia machozi ya watanzania wanaoonewa mbona MUNGU unawajua na hushindwi na udhalimu, tuokoe wanyomge wa Tanzania.
 

Forum statistics

Threads 1,275,229
Members 490,947
Posts 30,536,252