Inatia Huruma kwa Marehemu na Muuaji Pia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inatia Huruma kwa Marehemu na Muuaji Pia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mfumwa, Dec 27, 2008.

 1. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndugu wauana kwa Ugomvi wa kuangalia Luninga


  12/26/2008 5:07:48 AM
  MFANYAKAZI wa bustani, Innocent Elihuruma [19] wa Mikocheni B, Dar es Salaam amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la kumuua ndugu yake Nuru Isack katika ugomvi wa kuangalia luninga.
  Inspekta wa polisi Nassoro Sisiwaya aliiambia Mahakama kuwa kosa hilo lilitendeka Desema 19,mwaka huu, nyumbani alipokuwa anafanyia kazi mtuhumiwa eneo la Mikocheni B, majira ya saa mbili usiku.

  Alisema wakiwa na ndugu yake ambaye ni marehemu wakiangalia luninga ulizuka ugomvi uliotokana na aina ya kipindi cha kuangalia ambapo kila mmoja alikuwa anataka kuangalia kipindi alichokuwa anakihitaji, ambao ulisababisha kifo hicho.

  Alisema mtuhumiwa alimpiga marehemu teke la shingo lililomwangusha chini na kumwongezea teke linguine katika sehemu za siri lililomuua kabisa.
  Hata hivyo ilielezwa kuwa mara baada ya mtuhumiwa kuona amekwisha ua alimchukua marehemu na kumficha katika chumba kimojawapo walipokuwa wanaishi.

  Ilielezwa kuwa aliporudi mama mwenye nyumba mtuhumiwa aliendelea kuuficha mwili wa marehemu pasipo kumueleza mtu yoyote kwa muda wa siku mbili.

  Kutokana na hali hiyo iliweza kumshinda mtuhumiwa aliamua kutoroka, na tajiri yake alikuwa ameeenda kazini na kutoweka sehemu isiyojulikana, ndipo wakati yupo barabarani ghafla alikamatwa na polisi na kupelekwa kituo cha Oysterbay.

  Na kutokana na kosa alilolifanya la mauaji hakutakiwa kujibu lolote kuhusu shtaka hilo wakati akisomewa shtaka hilo mahakamani na hadi hapo atakapofikishwa katika Mahakama Kuu kujibu shtaka hilo na kesi imeahirishwa hadi hapo January 7, mwakani.

  Na Chondoma Shabani, Dar es Salaam
  Souce: Nifamishe.com
   
 2. c

  capuchino Member

  #2
  Dec 27, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakimu mkenjwa haki zenu hizo
  mmwagie chache kama 30 tu ...akukusudia jamani....
  R.i.p. Marehemu
   
Loading...