Inatia Hasira!

Rudini Bongo kuziendesha hizo wizara.
Mnafikiri mkikaa kwenye viota vya wenzenu nani atawaendeshea nji hii kama mnavyotaka?
 
Hahahaaa si bora hizo? Huku wamewekz taa za barabarani uhasibu na chang'ombe, zimewaka kwa muda wa wiki moja tu.....

Wanatuacha tugongane wenyewe tufe wapunguze population



...Mkuu mambo yameanza kigoma...Wameweka taa za barabarani zinawashwa pale anapokuja baba Riz tu otherwise zipo tu kama minazi ya kilwa!!....
 
Ndugu mpendwa unachokiona SA kimetolewa hapa hapa Tanzania. Tanzanite inapatikana Tanzania tu. Haya ni madini ambayo yanauzwa ghali ile mbaya nje ya Africa na yako femous sana. SA inachimba inabeba na udogo wetu inauza kwa jina lake then wanajenga taifa lao. Vilaza Watanzania tunaambulia kilio, huku rais wetu DHAIFU akiwachekea na kuwa ghaia bure. Kweli ipo siku hii CCM tutaizika na manyoya yake na huyu chekacheka anayejidai kuingoza huku taifa letu likiangamia mchana wa jua. Watanzania tumeonewa, tumaibiwa, tumenyanyaswa na ujinga wetu wenyewe ya kutosha. Tunalia huku madini yetu yakinyanyuliwa na udongo. Bandari zetu zinauzwa na walafi hatuwezi kusema kitu eti serikali. Kwa nini tusijiundie serikali inayowajibika? Matumbo tu na ma V-8? We can do better than that!
 
Tunawachagua wajinga kwa asilimia kubwa watuongoze kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa, na matokeo yake ndiyo hayo. Ukiwasikiliza viongozi walio wengi utagundua tu kuwa mawazo yao ni ya kipuuzi tu lakini wanashangiliwa na kuheshimiwa kwa ushabiki wa kizuzu (mfano mzuri unapatikana bungeni).
Tunahitaji kuwa na mawazo yanayolenga maendeleo kuanzia ngazi ya chini hadi juu na kuyatekeleza kivitendo vinginevyo tutakuwa tunatamani na kujilaumu wakati wenzetu wanazidi kusonga mbele.
Dunia ya leo siyo ya maneno ila ni ya vitendo na wakati mwingine waweza kutoa maneno yanayowafurahisha watu lakini matendo yako yakawa kinyume chake kwa kuwa matendo ndiyo yanayokuletea faida halisi na ya moja kwa moja!
 
Nimependa sana argument yako Mku.
 
Mkuu
ungetusaidia zaidi kwa kuchana ganda lako chooni fasta...ningeona usemi huu mzito na umeuchukulia hatua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…