ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 620
- 1,543
Hoja binafsi kuhusu kuundwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza vitendo vya utekaji na uteswaji imekataliwa Jana.
Hata hivyo, tutaendelea na hoja hiyo wiki ijayo baada ya mapumziko ya Pasaka ambapo Waziri mwenye kuhusika na Usalama wa Taifa ataleta hoja ya makadirio ya matumizi ya Idara hiyo.
Tunataka Idara ya Usalama ifanyiwe marekebisho makubwa ikiwemo kuvunjwa na kuundwa upya. Wananchi tunaomba mtuunge mkono kwenye ajenda hii ya kuufumua Mfumo wetu wa Usalama wa Taifa ili kuunda Idara inayosimamia Usalama na Maslahi ya Taifa badala ya Idara ya kuteka na kutesa watu.
Unakuwaje na Rais anayeingia field Mwenyewe kukamata mchanga wa dhahabu na kuunda Kamati 2 kuchunguza jambo moja wakati Usalama wa Taifa wapo? Kungekuwa na Usalama wa Taifa imara pasingekuwa na mambo kama haya. Lakini Kwa kuwa usalama unahangaika na watu na kuwateka mambo ya msingi ya nchi yanakosa usalama.
Tusichoke kutaka mabadiliko makubwa ya Idara ya Usalama wa Taifa.