Inakuaje wanaachwa wanakufa?

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
6,632
Reaction score
8,452
Hebu tujiulize kwa pamoja. Inakuaje wagonjwa wenye uwezo wa kutibiwa na wakapona na kuendelea na maisha yao, wanaachwa wanakufa kisa hawana uwezo wa kulipia gharama za matibabu?

Kwanini kuwe na budget za kununua vifaa vya kivita kwaajili ya kulinda usalama wa raia na mali zao huku hatuna budget za kununua dawa za kuwatibu hawa watu tunaowanunulia mavifaru yawalinde?

Haiingii akili eti vyama vya siasa na chaguzi zinawekewa ruzuku na budget kubwa huku uhai tukiuacha upotee!!!

Tuna wabunge ambao hawawezi hata kuliona hili wakaokoa maisha ya watu wengi ambao hawana uwezo wa kulipia gharama za matibabu.

Wananchi kutibiwa bure inawezekana maana hela hazitoki mifukoni mwa mtu yeyote bali ni kodi zao wenyewe. Ifike mahali tujue thamani ya uhai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…