Eng_mudiabd
Senior Member
- Mar 20, 2016
- 145
- 83
Kipindi cha nyuma serikali ilitoa bei elekezi ya sukari nchini kuwa @ TSh 1,800 na kuzuia kuingiza sukari kutoka nje ili viwanda vyetu viweze kuzalisha sukari ya kutosha.
Nahisi hii ilitokana na ushauri aliopewa Mh Rais na washauri wake kuwa viwanda vyetu vinauwezo wa kuzalisha sukari ya kutosha na kukidhi mahitaji ya watanzania.
Baadae hali ikawa mbaya bei ya sukari ikapanda zaid mpaka sehemu nyingine inakadiriwa kufikia @ TSh 3000 kwa kilo moja.
Hali imezidi kuwa mbaya na Waziri mkuu alitoa tamko bungeni kuwa wameagiza sukari kutoka nje ili kunusuru hii hali na hata Mh Rais akiwa Babati kwenye ziara yake alisema wamegiza sukari kutoka nje.
Swali la kujiuliza, wakati wanazuia sukari kuingiza sukari kutoka nje hawakuliona hili tatizo kama linaweza kutokea? Walifanya upembuzi yakinifu ili kujua uwiano wa kiwango cha sukari kinachozalishwa na viwanda vyetu vya ndani na mahitaji ya watanzania?
Kwa maamuzi yao hayo ya kuzuia kuingiza sukari Bila kufanya uchunguzi na kujipanga na kufanya watanzania wapate shida kwa kukosa sukari na kupanda kwa bei ya sukari, Je Rais na serikali yake inafaa watuombe msamaha watanzania kwa kosa lililotokea?