Inaelekea mapepo huwa yanaogopa sana sauti kubwa za spika

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Wadau!
Kuna huu mtindo Wa siku hizi makanisa mengi kufungwa system kubwa ya mziki kama disco!
Nimejaribu kuwaza hivi mchana au usiku wa manane Mchungaji kuhubiri Kwa sauti kuuubwa kupitia kwenye spika je nini lengo lake?
Hivi kanisa likiamua kuweka spika za sauti ya kusikika Kwa wasitani tu je mapepo hayatatoka?
Haya masipika ya siku hizi kanisani yanafaida gani? Tena hadi usiku jamani?
Kwani Mchungaji asipotumia mike au sauti ya kufoka kwenye spika ataonekana hajui kuhubiri?
Nawaza hapa sipati majibu kabisa!
"Mungu angekuwa anasikia kupitia spika, basi viziwi wasingekuwepo"
OMBENI KISTAARABU JAMAN MUNGU ANASIKIA HIZO ZINGINE NI ANASA TU.
 
Mbona hamuongelei baa na madisko au kwavile niwashilika huko vumilia tu mkuu
 
Naomba mleta thread utambue kuwa

Asili ya muziki ni mbinguni, ambapo malaika wanaendelea kumsifu na kumwabudu Mungu Mwenyezi.

Ni jambo la maana sana Injili ikahubiriwa kwa sauti kubwa ya kutosha ili wewe mwanadamu usiekwenda ktk makusanyiko hayo nawe upate kuisikia Injili hio ili yamkini uweze kuupokea WOKOVU ulio ktk damu ya KRISTO YESU.

Na kama sauti za Mahubiri huwa zinakukera, huo ni uthibitisho kuwa uko upande wa pili (wa ibilisi-shetani) stuka chukua hatua!

KARIBU KWA YESU UPATE RAHA AMBAYO HUJAWAHI KUIFIKIRIA!.
 
Hapo zamani hakukuwa nahayo maspika naneno LA mungu lilikuwa linapenya ndani ya mioyo ya watu.. Lakin skuiz makelele ndio mapepo yatoke.... Vizazi vya nyoka vivyo saiv ujanja ujanja tu... Mbinu yakupata utajiri.. Naakipata anaanza kumshukuru mungu kwa kumpa utajiri badala yakuwashukuru wale wanaohangaika watoe sadaka na mafungu ya kumi... Tena kwenye sadaka... Ukitaka kujua kama huduma nimbovu basi SKU waumini wasitoe sadaka WA fungi lakumi.. Wakwanza kulalamika niviongozi WA kanisa... Eti nao hali mbaya...
 
VIPI VIPAZA SAUTI VYA KIISLAMU NAVYO VINAKERA SANA KUANZIA SAA 7 MCHANA ,SAA 10 JIONI, SAA 2 USIKU NA SAA 11 ALFAJIRI WANAKERA SANA HAWA JAMAA
 
VIPI VIPAZA SAUTI VYA KIISLAMU NAVYO VINAKERA SANA KUANZIA SAA 7 MCHANA ,SAA 10 JIONI, SAA 2 USIKU NA SAA 11 ALFAJIRI WANAKERA SANA HAWA JAMAA
wale wenzetu ni dk 5 tu wamemaliza....sasa haya makanisa ya kilokore yakianza saa 5 usik mpaka asubuh mkuu...usiombee kukaa karibu na kanisa utajuta mkuu
 
VIPI VIPAZA SAUTI VYA KIISLAMU NAVYO VINAKERA SANA KUANZIA SAA 7 MCHANA ,SAA 10 JIONI, SAA 2 USIKU NA SAA 11 ALFAJIRI WANAKERA SANA HAWA JAMAA
Vipaza sauti vya waislamu ni kwa muda nfupi siyo kwa walokole ni usiku kucha na mchana kutwa watu hatulsli kwa mikelele ya kuwaombea wagonjwa na mizik i ya sauti kali!! Inakera sana!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom