Inadaiwa mwenyekiti BAVICHA Geita hajulikani alipo

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Mwenyekiti wa BAVICHA jimbo la Geita Vijijini, Mbeshi Paulo, ameripotiwa kutoweka katika mazingira ya utata baada ya kuchukuliwa na watu waliodaiwa kujitambulisha kuwa askari wa Polisi.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) Taifa, Wakili Deogratius Mahinyila, kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa X amedai kuwa tukio hilo lilitokea mnamo 18 Julai 2025 baada ya gari kufika nyumbani kwa Mbeshi na kumchukua kwa maelezo kuwa walikuwa ni askari wa Jeshi la Polisi.

Habari zaidi zinasema familia yake haijui alipo, licha ya kufanya juhudi za kumtafuta katika vituo mbalimbali vya Polisi bila mafanikio.

Screenshot 2025-07-20 124615.png
 
DAH wahuni wameanza TENA ILA HIZI tabia nmezikemea juzi Leo wameanza TENA itafika hatua tutaanza kupigana risasi hayo mambo SI mazuri yakemewwe
 
Kwahio mkiwaua hivo mnapata nini? Au kafara
 
Nmemfikiria Ben SAA nane hakika maumivu wanayo pitia wazazi na NDUGU na watoto natamani SIKU MOJA KIONGOZ mkubwa limpate JAMBO tuheshimu damu za WATU. Wazazi wanakuza kwa uchungu wanajinyima kula mtoto ale asome ajitegemee ana KUJA MTU TU kuua inasikitisha sana
 
Mwenyekiti wa BAVICHA jimbo la Geita Vijijini, Mbeshi Paulo, ameripotiwa kutoweka katika mazingira ya utata baada ya kuchukuliwa na watu waliodaiwa kujitambulisha kuwa askari wa Polisi.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) Taifa, Wakili Deogratius Mahinyila, kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa X amedai kuwa tukio hilo lilitokea mnamo 18 Julai 2025 baada ya gari kufika nyumbani kwa Mbeshi na kumchukua kwa maelezo kuwa walikuwa ni askari wa Jeshi la Polisi.

Habari zaidi zinasema familia yake haijui alipo, licha ya kufanya juhudi za kumtafuta katika vituo mbalimbali vya Polisi bila mafanikio.

Huu ushenzi haujakoma tu ?!
Mbona wengine wamejimilikisha uhalali wa Utanzania !!.

Kwanini nembo ya police iendelee kutumika kuumiza watu ?!.
 
Lakini huu unakuwa sasa ujinga wa watekwaji, kwani hakuna balozi mmenichukua kinguvu? Bora nipambane mniulie nyumbani
 
Back
Top Bottom