Inachukuwa muda gani tangu mwanamke ajifungue hadi kupata tena ovulation?

garson

Member
Sep 15, 2015
45
15
Habar ya mchana ndugu zangu. Naomba kufahamu inachukuwa muda gani tangu mwanamke ajifingue hadi anapoanza tena ovulation. Au ni muda gani tangu mwanamke ajifungue unapita hadi pale anapoweza kushika ujauzito?
 
Habar ya mchana ndugu zangu. Naomba kufahamu inachukuwa muda gani tangu mwanamke ajifingue hadi anapoanza tena ovulation. Au ni muda gani tangu mwanamke ajifungue unapita hadi pale anapoweza kushika ujauzito?
Inachukua wiki 10 kama mama hanyonyeshi, ila kama ananyonyesha inachukua wiki 20 (miezi 5) inaweza ikazidi au kupungua kidogo
 
Hakuna jibu sahihi kwa wote
Inategemea n.a. fertility ya mama, kunyonyesha au kutonyonyesha
WaPo kinamama wakijifungua hedhi zao zinarudi the very next month anyonyeshe asinyonyeshe

Kinachofahamika ni kwamba unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama pekee unachelewaesha hedhi kwa maana ingine ni njia mojawapo ya uzazi wa mpango
Tambua hali yako ya hedhi kurudi mwanamke unatofautiana n.a. mwenzio
Wenzetu walioendeleawanavipimo kuweza kujua mabadiliko ya hormone kimwili kujua mama utaona hedhi lini sisi bado tupo nyuma kitechnologia
 
Dah swali la msingi sana hilo, kuwa makini mzee usije mtandika mimba wakati mtoto ana miezi 2.
 
Kama ananyonyesha kisawasawa ni njia nzuri tu ya uzazi Wa mpango mfano mwanamke anaweza kunyonyesha mtoto kwa muda Wa miezi sita bila ya kumpa chochote mtoto....yaani ni maziwa ya mama tu. Hii inasababisha kutawala kwa aina moja ya hormone na kuzuia kabisa ovulation kwa kipindi chote ambacho mama atakua ananyonyesha lakin anapoacha tu basi kunauwezekano Wa mzunguko wake kurudi kawaida. Kuwa makini kwa muda huu ipo chance ya kumpa mama mtoto mimba kwa kuwa kukoma kwa ovulation kwa njia hiyo uhakika wake sio asilimia mia moja. Wapo wanawake wanakua na amenorrhea hata kwa Mwaka mmoja na zaidi kipindi chote cha kunyonyesha.
 
Ovulation inakuja baada ya kumaliza arobaini ina depend,nakwambia ivo kwasababu dada angu alizaa mtoto ,alipozaa baada ya mwez mmoja akasema nataka kwenda kwa mume wangu arobaini inshakwisha,siku aloenda kwa mumew ndo siku alobeba mimba,Ilikua aibu tu na kitu cha kustaajabisha,ikabiidi alee tu na kashazaa sasa
 
Hakuna muda maalumu, wengine miezi 2, 3 5 wengine hadi miaka 2.
 
Back
Top Bottom