Inachekesha lakini kweli.....

Inachekesha lakini kweli.....

Candy kisses

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
297
Reaction score
211
Kumpenda mtu asiyekupenda ni kama mwanafunzi wa HGL kufaulu mtihani wa Hesabu,inabidi uwe na moyo mgumu kama bati la Alluminium..

Kwakweli inabidi kabla hujafall mzima mzima kama furushi la nguo chafu upime angalau kuna lita ngapi za Love kwenye tenki la huyo mtu,unaweza ukaanzisha safari ya Sumbwanaga kumbe gari ina nusu lita,ngoma itabuma hapo kimara Korogwe...

Unajitahidi we kujishaua,kumuonyesh...a unampenda,unarudi home na zawadi, unamletea Ma-Apple anakwambia ye anapenda Parachichi,Ukileta Sausage anasema anataka mayai,mwishowe utamletea mayai atakwambia anapenda mayai viza,ilimradi tu vululu vululu...Najua kuna wengi tu mnateseka kupenda msikopendwa maskini,mnajitahidi kushow Love weee mnakumbana na Steringi wa Vampire Diaries,somo halieleweki,unabaki na hope tu Labda...Labda One day atakupenda.
Ni kama vile mko Airport mnasubiria Bajaj za kwenda Salasala,utakesha hapo,zinatua Ndege tu
 
Mbona umemlete rafiki yako wa FB hadharani kwa kumtaja jina hapa JF? Ulimconsult? Au seth giovanni ndiyo wewe mwenyewe?

sijaconfirm kama ni yeye au lah, ila that post, yeye ndo uwa anaandika hivyo, ana fan page ina watu weeengi... na tunafahamiana miaka kedekede... nimeona tu nikajua ni yeye hata nilivyogoogle nikaona makala ni ya blog yake
 
Yes ni Seth n sio vibaya kushare ideas ila mhusika ange acknowledge katoa wapi.
 
Huyo wa kupenda mayai viza nae sasa lol!
Mletee tu sianayapenda yeye bana
 
mwana kama umenigusa vile na kama ulikuwepo kwenye masahibu yangu
Kumpenda mtu asiyekupenda ni kama mwanafunzi wa HGL kufaulu mtihani wa Hesabu,inabidi uwe na moyo mgumu kama bati la Alluminium..

Kwakweli inabidi kabla hujafall mzima mzima kama furushi la nguo chafu upime angalau kuna lita ngapi za Love kwenye tenki la huyo mtu,unaweza ukaanzisha safari ya Sumbwanaga kumbe gari ina nusu lita,ngoma itabuma hapo kimara Korogwe...

Unajitahidi we kujishaua,kumuonyesh...a unampenda,unarudi home na zawadi, unamletea Ma-Apple anakwambia ye anapenda Parachichi,Ukileta Sausage anasema anataka mayai,mwishowe utamletea mayai atakwambia anapenda mayai viza,ilimradi tu vululu vululu...Najua kuna wengi tu mnateseka kupenda msikopendwa maskini,mnajitahidi kushow Love weee mnakumbana na Steringi wa Vampire Diaries,somo halieleweki,unabaki na hope tu Labda...Labda One day atakupenda.
Ni kama vile mko Airport mnasubiria Bajaj za kwenda Salasala,utakesha hapo,zinatua Ndege tu
 
HGL kufaulu hesabu ni breaknews?? Ngoja waje wenyewe uone povu lao..
 
acha kujifanya mgeni wakati nyie ndo mnaongoza kwa kunyanyapaa wadada na kuwapa stress za ajabuajabu

bi dada nashukuru mungu ameniepusha unyanyasaji wa kila aina, hilo najiamini mwenyewe...
 
Back
Top Bottom