In the news:Benki yas FBME yasaidia yatima

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Benki ya FBME yasaidia yatima
Tuesday, 07 September 2010 20:06

Vicky Kimaro


KITUO cha kulelea watoto yatima cha Malaika kilichopo wilayani Mkuranga kimepokea misaada ya vyakula mbalimbali vyenye thamani ya Sh 500,000 kutoka Benki ya FBME ya jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi misaada hiyo, Ofisa huduma kwa wateja wa benki hiyo, Doroth Buki alisema benki hiyo ni sehemu ya jamii, hivyo wanawajibu wa kurudisha na kutoa sehemu ya faida kwa jamii.


"Huu ni mwendelezo kwa FBME katika mipango mingi ya kusaidia jamiii, hasa wale wanaoishi kwenye mazingira hatarishi."alisema Buki.


Naye mkurugenzi wa kituo hicho Najma Manji alisema kituo chake kina jumla ya watoto 33 ambao wamewapata kutoka sehemu mbali mbali ikiwemo ustawi wa jamii.


"Makao Makuu ya kituo chetu yapo Mkuranga, lakini makao makuu yetu yapo Kinondoni na ndipo tunapowapokea na wanakaa hapa kwa miezi minne kwa ajili ya uchunguzi kabla ya kuwahamishia Mkuranga."alisema Manji


Alisema baadhi ya watoto wamekuwa wakiletwa kwenye kituo hicho wakitokea mtaani, wengine ustawi wa jamii na wengine ni wale ambao wanatelekezwa na wazazi wao wakiwa wachanga.


Hata hivyo Manji ameitaka jamii kutambua kuwa jukumu la kuwalea watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi ni la kila mmoja na kuiomba jamii ijitoe kwa watoto hao kwa kuwapenda na kuwasaidia vitu mbali mbali kama walivyofanya benki hiyo ya FBME kwani kwa kufanya hivyo kunawapunguzia makali yamaisha.


Alisema watoto hao wanahitaji upendo, faraja na malezi bora kama walivyo watoto wengine
 
Back
Top Bottom