In the name of love

Maisha ni kuchagua na kuamua,
namuona mwanaume kwamba ni binadamu kama nilivyo mimi,
anachokipata pengine mapata zaidi yake,
kwa nini nilazimishe anipatie kile anachokipata ilhali ninaweza kutumia nilichonacho na nikaweka maisha yetu/yangu sawa?
Wanawake wengi wanapumbazwa na maneno ya vijiweni,mtaani wanakosa kuwa na maamuzi yaliyo sahihi na hii ndiyo sababu inayofanya baadhi ya wanawake kuwa tayari kunyanyaswa ilimradi apate alichoacho mwanaume.
uko peke yako kati ya mia! haujaona thread ya miss chagga ?
 
Last edited by a moderator:
mi nimemsikiliza huyu jamaa nimesoma weeeee nimeona anampigia gita mbuzi unajua unaweza ukapenda kiukweli toka moyoni ila uliyempenda yeye hakupendi kiukweli toka moyoni, na akikutenda huyo tu sumu yake ni kali itawaumiza wajao wote!!!!
ningekuunga mkono kuwa tuwe na michepuko mingi ila tuwajali wake zetu hapo ningeona point....!!!!
 
Sikuizi material are being loved and people are being used... ukiwa na munot utaona kila mtu anakupenda... utajiona we hansome bt penz la kweli sikuiz ngumu sana... kwanza watu wanaogopa kupenda... ni kuviziana tu uishiwe ule kibut
 
Historia inasema wanawake zamani walikuwa hawasomeshwi kazi yao kubwa ilikuwa ni kulea watoto. Ndo maana wazazi wenu wanamaadili sio sawa na kizazi cha sasa.

Jukumu la mwanaume lilikuwa ni kumtunza mwanamke na kutunza familia. changamoto ikaibuka ya mfumo dume wanawake wakajanjaruka na haki sawa. Wakaanza kupelekwa shule vipaumbele vyakutosha kupunguza mfumo dume.


Wanawake wenyewe ndo walitaka haki sawa ili kujipatia kipata kukwepa mfumo dume. Sasa mmepata fursa, kazi mnafanya wengine wanafedha kuliko wanaume bado mnataka kugharamiwa kila kitu na pesa zako unapeleka wapi?


Mnaoingia kwenye ndoa na mliopo kwenye ndoa mkiwa na dhana ya kugharamiwa kila kitu na mwanaume/mme maendeleo utayasikia kwa wenzako.

Mkishakuwa kwenye mahusiano/ndoa you have to work as a team. Me leta pesa mezani Ke the same pangeni bajeti, mbona maendeleo yatakuja haraka, miradi itaongezeka. Pesa itapatikana na kazi ya pesa kugaramia waliotafuta.


Nyie wanawake wa JF fikirieni na wenzi wenu jinsi ya kuongeza pesa. Sio kila kukicha kulaumi wanaume hawawa garamii/wabahili.
 
hivi kuna kitu kinachoitwa mapenzi ya kweli siku hizi?!
Siku zipi katika maisha yako yalikuwepo na unadhani yamekwenda wapi sasa?
Na kwa kauli yako hiyo ina maana unaamini kuwa yalikuwepo kwanini ishindikane sasa ama leo?

Kufanya ni kutaka na kutaka ni kuamua, Hapana shaka unaweza ukawa nayo hata wewe.
Ila sasa kama ma-negativity yametawala kichwa yako inakuwa shida kwelikweli hata kuamini tu kuwa yapo,
Lakini kiukweli yapo tena saaana tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…