Imenitokea: TRA=Rushwa, la sivyo wanakukomoa na hamna utapo wapeleka

ramses2

Member
Jan 19, 2016
47
29
TRA ni wezi wenye chuki binafsi na wenye lengo la kukomoana. Serekali imewawekea njia thabiti za wao kuutawala huo mchakato mzima wa wizi na uonevu. Kutumia njia halali ni sawa na kutangaza vita nao. Kwa hali yoyote ile utashindwa, kwa sababu wanao support toka kwa Mh. Magufuli. Hoja sio kutumbuwa jipu bali ni kutafuta kinacho sababisha majipu kujitokeza.

Akitoka kuyakausha majipu yote leo leo basi dunga sindano ya antibiotic na yatakauka. Maana yangu badili system. majipu ni matokeo ila ugonjwa upo ndani kwenye damu. Wanasiasa wamejikita kwenye biashara. Sasa hawataki mtu yeyote kuleta biashara yake hapa, labda awe anawafanyia kazi wao.

Sintoweza weza kumshauri mtu alete mzigo wake Tanzania kamwe. Na nikiwaza kurudi basi nitarudi na adabu kwenu TRA. Nitawapa RUSHWA mnayoitaka ili msinikomoe kama safari hii. Na kama haitowezekana basi Tanzania itakuwa imempoteza muwekezaji toka nje ila mzawa mwenye huruma na ndugu zake.

Msimlaumu tu asiye lipa kodi bandarini, ni busara kuchunguza kwa nini hajalipa? Kutokana na yanayo nikuta nitasema watanzania walimuelewa Mh. Magufuli aliposema HAPA KAZI TU = HAPA UZEMBE TU kama kawaida. Kila step ya TRA na bandari ambayo inachukua tu madakika au saa, imewachukuwa siku tatu tatu. Kulipia ushuru wa uonevu na kupewa release imechukuwa siku mbili. kulipia bandari pia siku mbili, gharama za storage zinazidi tu kuongezeka.

Huwezi kuwa shuhuli moja vitengo 50 alafu useme unapambana na rushwa. Wewe ndio mwenye kusababisha. System mmeifanya kuwa very complicated. Hata haki nanyimwa alafu sijui niende wapi. Na anayeninyima ndo ananiambia ukipinga utaumia zaidi. Mzigo kisheria una exemption ila natozwa kodi ya anasa. Hivi watanzania mmelogwa? Kwa nini kuweka sheria alafu mzidharau?

Nyie ni binadamu wa aina gani, ni rahisi kuyamaliza yote haya kama nchi itapata head of state asiye kuwa corrupt. Naona sasa hivi nchi ina laana na inahitaji nusura za Mwenyezi Mungu. Na hoja sio kuyatumbuwa majibu, jaribu kuyatibu majipu.

Huwezi piga keeler uchumi wa viwanda huku kodi yako ni zaidi ya nchi zenye viwanda. Hivi unaitaji PhD kujuwa kwa nini viwanda vilitoka Ulaya na Marekani kwenda China? Leo viwanda vina muelekeo wa kuja Africa ila kwa hali hii sio hii Africa ya Tanzania. Atakae kuja hapa sio muwekezaji halali, atakuwa ni mwizi/tapeli anaye shirikiana na viongozi wenu.

Tanzania imebarikiwa kweli sio siri ila viongozi wana upeo ulio finyu zaidi. tofauti na hivo Dar ingelikuwa zaidi ya Dubai. Kagame alisema akipewa tu bandari ya Dar, atawalisha watanzania wote. Tusi kubwa kwa wasio ona mbali ila ukweli na ukumbusho kwa wanao ona mbali na kulipenda taifa hili.

ASANTENI SANA KWA KUSOMA.

Mungu awabariki manaake Tanzania ilisha barikiwa tayari.
 
Back
Top Bottom