the grate
JF-Expert Member
- Sep 24, 2011
- 204
- 36
habari zenu wana jf.. Jana kunakitu kimenikera sana, nilipokuwa nikitoka kazini mida ya sa4 nilipita eneo fulani nikakuta vijana kama sita wakiwa mamemfunga kijana mwingine kamba miguuni na mikononi huku wakimpiga kama mwizi nilipojaribu kusogea kuuliza kuna nini wakajibu "huyu jamaa kamchukulia msela wetu demu" nikajitahd kuamua huku nikiwatsha naita polis kweli wakamuacha lakini jamaa ameumia sana na nilipomuhoji akasema yule demu ndo alimfata akamtaka wawe wapenzi. Hadi sasa jamaa yuko hospitali anauguza majeraha. Hivi wenzangu ni halali kuumizana kwa ajili ya mapenzi? Naomba kuwasilisha