figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
1. Hisa ni nini?
Hisa ni sehemu ya umiliki wa kampuni. Hivyo hisa moja inawakilisha asilimia ndogo ya umiliki katika kampuni. Kama kampuni ina hisa milioni moja na mwekezaji anamiliki hisa 10,000, mwekezaji huyu anamiliki 1% ya kampuni. Mwekezaji anayenunua hisa basi ananunua haki ya kumiliki kampuni. Stahili za mwenye hisa ni pamoja na kushiriki katika kutoa maamuzi ya kampuni katika mkutano mkuu wa wanahisa na kupata gawio litokanalo na faida. Ana haki pia ya kuuza hisa zake kwa faida pale ambapo kuna ongezeko la thamani ya hisa.
2. Gawio ni nini?
Gawio ni malipo yanayofanywa na kampuni kwa wanahisa kutokana na faida ya kampuni. Malipo haya yanapendekezwa na wakurugenzi na kuidhinishwa na mkutano mkuu wa wanahisa. Gawio linaweza kulipwa kutokana na faida ya mwaka husika au malimbikizo ya faida za nyuma. Gawio linaweza kulipwa kwa fedha taslim au kwa kuwaongezea hisa wanahisa.
3. Hatifungani ni nini?
Hatifungani ni hati ya deni ambalo kampuni au serikali huwakopa wawekezaji kwa makubaliano maalumu na kuwalipa riba na marejesho baada ya kupevuka kwa hatifungani hiyo. Mwenye hatifungani anastahili kulipwa riba (kwa kawaida ni kila miezi sita) na kurudishiwa mtaji wake hatifungani ikishapevuka. Pale ambapo kampuni inafilisika, wanaomiliki hatifungani wana haki ya kulipwa pesa zao kabla ya wale wanaomiliki hisa.
4. Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ni nini?
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ni taasisi ya serikali iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Uchumi iliyoanzishwa na Sheria namba 5 ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya mwaka 1994 ili kusimamia na kuendeleza masoko ya mitaji hapa Tanzania. Majukumu makubwa ya Mamlaka yameainishwa kwenye kifungu namba 10 cha Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana. Majukumu hayo ni pamoja na: a) Kuanzisha na kuendeleza masoko ya mitaji Tanzania; b) kuidhinisha uanzishwaji wa masoko ya hisa na mifuko ya uwekezaji wa pamoja, na kutoa leseni kwa wataalamu wa masoko ikiwa ni pamoja na madalali, wachuuzi, wawakilishi wao, washauri wa uwekezaji, n.k. c) Kusimamia masoko ya mitaji pamoja na wataalamu wote wanaohusika na utendaji wa masoko hayo; na d) Kuishauri Serikali kwenye masuala yote yahusuyo masoko ya mitaji na dhamana.
5. Soko la hisa la Dar-es-Salaam ni nini?
Soko la Hisa ni soko ambalo huwezesha hisa, hatifungani na dhamana zingine zilizoorodheshwa katika soko hilo kuuzwa na kununuliwa. Bidhaa hizi huitwa dhamana au kwa lugha ya kigeni (securities). Soko la hisa hapa Tanzania limeanzishwa mwaka 1996 kama kampuni binafsi yenye dhima (limited by guarantee); kwa maana ya kwamba wanachama wa soko hawatakiwi kuweka mtaji wowote. Mwanzoni kulikuwa na wanachama 11 ambao ni madalali wa soko la hisa pamoja na wawekezaji wakubwa (Institutional investors). Soko la hisa lilianza kazi zake rasmi mwezi April mwaka 1998 wakati hisa za TOL Ltd zilipoorodheshwa na kuanza kuuzwa na kununuliwa. Soko la hisa ni soko ambalo linajiendesha lenyewe likisimamiwa na Baraza la Wadhamini (DSE Council). Kwa sasa lina wanachama 27.