Imani za kibongo

Imani za kibongo

IrDA

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2010
Posts
745
Reaction score
361
1. Mvua ikinyesha wakati jua linawaka……….simba anazaa
2. Ukinywa maji ya nazi……utapata busha
3. Mtu akikuruka…..utakuwa mfupi
4. Usiokote chakula kilichodondoka…..shetani amekila
5. Mtu akikuuma, pka mavi ya kuku alipokuuma…meno yake yataoza
6. Ukifagia usiku…unafagia bahati
7. Uking’oa jino tupia juu ya bati…kunguru wakichukua watakuletea jingine
8. Ukimpiga mbayuwayu na manati chanjia damu yake unakuwa na shabaha
9. Ukivaa kiatu kimoja…titi la mamako litavimba
10. Mtu akisimama nyuma yako wakati umekaa anakunyonya damu


Na wewe ongezea.....
 
mvua ikinyesha cku ambayo Simba SC. inacheza, Simba inashinda.
 
Back
Top Bottom