nilianzisha uzi kuhusu Kiba nilimshauri akaimbe kaswida aache tabia yake ya kutembelea nyota ya DaiJamani sijui wenzangu mnaofatilia Bongo fleva mnaonaje hili!
Hivi ulishawahi kusikiliza vema nyimbo za Ally Kiba anazoimba sasa baada ya kutoa ule wimbo wa "Mwana" halafu ukajiuliza Diamond asingekuwepo huyu Kiba angekuwa kwenye level gani,hasa baada ya kusikiliza nyimbo za akina Ben Pol,Baraka, na Jux? Mimi naamini hao wote wangekuwa juu yake. Ally K alikuja juu baada ya kuibuka mwanzoni kisha akapotea na baadae bifu uchwara iliyotengenezwa na wachwara kati yake na Diamond ikamuweka vichwani na midomoni mwa wafuatilia Bongo fleva hadi sasa. Kwa maoni yangu naona Ally K ni kama Ray ma water alivyokuwa anatembelea nyota ya Kanumba!
Mkuu hao sio jamaa zangu,ila kwa kuwa nasikiliza pia bongo fleva,najaribu kupima ubora na uzuri wa nyimbo za hao jamaa sioni sababu ya wao kushindanishwa cz mmoja yuko mbele sana!Hawa jamaa zenu nao wana uhasama?,maana washabiki povu,pengine wenyewe wapo poa tu..
Hata yule jamaa aliimbaga na juma nature Tina lile tina mama! Tina lile tina wewe! Alivuma kabla hatujamjua Daimond. Kilichotokea ni kwamba Kiba ni kama yule kipofu kwenye filamu ya Yesu alivyobahatika kupitiwa na msamalia mwema akamrudisha mstarini.Ali Kiba alivuma kipindi hatumjui Diamond, akili yako chwara eti anatembelea nyota ya Diamond
Yaleyale mtu kajikadiria miaka mingi kuliko baba yake
Ha ha ha nishajua upo upande gani mkuu...poa pamoja.Mkuu hao sio jamaa zangu,ila kwa kuwa nasikiliza pia bongo fleva,najaribu kupima ubora na uzuri wa nyimbo za hao jamaa sioni sababu ya wao kushindanishwa cz mmoja yuko mbele sana!
Yani huwa siamini kama Ally K hawezi kutunga nyimbo nzuri, cjui ni nn kinamkuta. Sasa cjui ndo uwezo umefikia kikomo!!Nampenda Ally kiba ila kiukweli hafanyi vizuri, wimbo wa Aje wamejaribu kuupromote lakini hauvutii, ukijumlisha na huu aloimba na Baraka ndo hovyo kabisa,.. Kiba pliiiz imani tuliyonayo mashabiki wako ni kubwa hebu fanya kitu cha hadhi yako yani ni km tunakuforce kila siku unazidi kushuka