Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 227
- 246
Huwa kuna mstari mwembamba kati ya kujikweza na kutoa hamasa kwa watu wengine. Nikaamua kurejea kwenye hekima za wahenga. Kuna ambao walisema " Nyumba haijengwi na mtu mmoja" na wengine wakafikiria zaidi kwamba " umoja ni mshikamano na utengano ni udhaifu". Wengine wakatutahadharisha zaidi kwamba "Kamba hukatikia pabovu" yote hayo ukiyapitia unaona ni hekima zaidi ambayo ilijengwa kwenye soga zao na wenye akili wakaamua zitumike kama methali.
Mlimwengu mimi nataka nizungumzie uzuri wa Mwezi wa Ramadhan. Kila mtu anaelewa umuhimu wa mwezi huu kwa mtu anayeitwa muislamu haijalishi kipimo chako cha imani dhidi ya uislamu. Ni mwezi ambao ni kipimo cha mwanadamu kujitafakari kwa mahusiano yake na Mwenyezi Mungu. Ni mwezi ambao unahitaji sana msamaha, unahitaji kusali sana, unahitaji kutenda mambo mazuri ambayo hayaharibu utu wa mwenzako. Hii ndio siri kubwa ya mwezi huu na ikawe ya kuendeleza hayo mazuri kwa kipindi chako chote cha kuishi ulimwenguni.
Katika hili na lile kwenye miji ya watu, nikaona siyo mbaya nijisogeze na mimi kwenye nyumba ya ibada nikamuombe Mungu maana na mimi ni mdhambi kama wadhambi wengine na mimi ninahitaji fadhila za mola wangu. Nikaamua kujijengea tabia ya ikifika usiku nijisogeze masjidi, huko mwenda bure si mkaa bure kuna kitu nitaokota.Maana kwenye nyumba ya ibada ni sehemu ambayo matendo mazuri yanafanyika. Nitamuomba Mungu, nitasoma vitabu vya dini na nitasifu na kumtukuza mola wangu kwa ukubwa wake aliyo nao.
Hayo yote nimeandika zilikuwa porojo ila mantiki ya kuandika kwangu ni hili tukio. Wakati niko masjidi ikifika muda wa kula daku. Wote tunaamshana na kama kuna mtu alipitiwa usingizi anaamshwa. Ukiamshwa hujui unaenda kula nini. Picha inaanza watu wote hamjuani hata kwa majina ila mnatambuana kwa udugu kwa kuwa nyote ni waislamu. Mtaitana sheikh, mtaitana hustadhi, mtaitana maalim na majina yote ambayo ni mazuri hayamkwazi mtu, utadhani mnafahamiana kabla.
Hakuna ubaguzi kila mtu atapakua chakula chake na ambaye hana wala siyo shida.Na chakula kinawekwa sehemu moja na mnakula kwa pamoja Chakula kile mnakula kwa imani moja kwamba ni cha ndugu yenu. Huyo mtu hajui kapikia wapi? Hicho chakula kaweka nini? Lakini imani zenu ndio zinafanya wote muaminiane. Hutaona ubaguzi wa kiumri, ubaguzi wa kutaka kujua status ya mtu, ubaguzi wa kikabila na chembe yeyote ya ubaguzi. Mtasikilizana na mtakula pamoja na kisha mtashake hands kuonyesha mshikamano na umoja.
Hiki kisa changu nikarejea kwa mwanaharakati wa kimarekani ambaye aliitwa Malcom X. Alipambana na vita ya ubaguzi iliyokuwa ikiendelea Marekani dhidi ya watu weusi na weupe. Kwa ukubwa wa Mwenyezi Mungu baada ya kutoka kuhiji Makka. Alibadilisha msimamo wake wa mtazamo akaacha kuwachukia watu weupe kutokana na kile alichokutana nacho Mecca. Malcom X aliweza kuhubiri mazuri ya uislamu kwa kutoa ushuhuda wake kwamba aliacha kuwachukulia wazungu wote kama maadui, akasisitiza zaidi katika maisha yake yote hakuwahi kushuhudia ukarimu wa dhati na roho ya kweli ya udugu kama aliyokutana nayo Makka.Akahitimisha akaona dini ya uislamu inaweza kuwa mbadala ya kufuta ubaguzi wa rangi uliyopo Marekani.
Alishuhudia maelfu ya watu wakiwa Makka wakishirikiana pamoja kwa kula pamoja, kunywa pamoja na kusikilizana. Na hilo likampa funzo kubwa ya kutowachukia wazungu maana alivyokuwa Makka alikutana na wazungu wenye roho nzuri na upendo Huwa kuna mstari mwembamba kati ya kujikweza na kutoa hamasa kwa watu wengine. Nikaamua kurejea kwenye hekima za wahenga.
Kuna ambao walisema " Nyumba haijengwi na mtu mmoja" na wengine wakafikiria zaidi kwamba " umoja ni mshikamano na utengano ni udhaifu". Wengine wakatutahadharisha zaidi kwamba "Kamba hukatikia pabovu" yote hayo ukiyapitia unaona ni hekima zaidi ambayo ilijengwa kwenye soga zao na wenye akili wakaamua zitumike kama methali.
Mlimwengu mimi nataka nizungumzie uzuri wa Mwezi wa Ramadhan. Kila mtu anaelewa umuhimu wa mwezi huu kwa mtu anayeitwa muislamu haijalishi kipimo chako cha imani dhidi ya uislamu. Ni mwezi ambao ni kipimo cha mwanadamu kujitafakari na mahusiano yake na muumba wetu. Ni mwezi ambao unahitaji sana msamaha, unahitaji kusali sana, unahitaji kutenda mambo mazuri ambayo hayaharibu utu wa mwenzako. Hii ndio siri kubwa ya mwezi huu na ikawe ya kuendeleza hayo mazuri kwa kipindi chako chote cha kuishi.
Katika hili na lile kwenye miji ya watu, nikaona siyo mbaya nijisogeze na mimi kwenye nyumba ya ibada nikamuombe Mungu maana na mimi ni mdhambi kama wadhambi wengine na mimi ninahitaji fadhila za mola wangu. Nikaamua kujijengea tabia ya ikifika usiku nijisogeze kwenye masjidi, huko mwenda bure si mkaa bure kuna kitu nitaokota.Maana kwenye nyumba ya ibada ni sehemu ambayo matendo mazuri yanafanyika. Nitamuomba Mungu, nitasoma vitabu vya dini na nitasifu na kumtukuza mola wangu kwa ukubwa wake aliyo nao.
Hayo yote nimeandika zilikuwa porojo ila mantiki ya kuandika kwangu ni hili tukio. Wakati niko msikitini ikifika muda wa kula daku. Wote tunaamshana na kama kuna mtu alipitiwa usingizi anaamsha. Ukiamshwa hujui unaenda kula nini. Picha inaanza watu wote hamjuani hata kwa majina ila mnatambuana kwa udugu kwa kuwa nyote ni waislamu. Mtaitana sheikh, mtaitana hustadhi, mtaitana maalim na majina yote ya mazuri utadhani mnafahamiana kabla.
Hakuna ubaguzi kila mtu atapakua chakula chake na ambaye hana wala siyo shida. Chakula kile mnakula kwa imani moja kwamba ni cha ndugu yenu. Huyo mtu hajui kapikia wapi? Hicho chakula kaweka nini? Lakini imani zenu ndio zinafanya wote muaminiane. Hutaona ubaguzi wa kiumri, ubaguzi wa kutaka kujua status ya mtu, ubaguzi wa kikabila na chembe yeyote ya ubaguzi. Mtasikilizana na mtakula pamoja na kisha mtashake hands kuonyesha mshikamano na umoja.
Hiki kisa changu nikarejea kwa mwanaharakati wa kimarekani ambaye aliitwa Malcom X. Alipambana na vita ya ubaguzi iliyokuwa ikiendelea Marekani dhidi ya watu weusi na weupe. Kwa ukubwa wa Mwenyezi Mungu baada ya kutoka kuhiji Mecca. Alibadilisha msimamo wake wa mtazamo akaacha kuwachukia watu weupe kutokana na kile alichokutana nacho Mecca.
Malcom X aliweza kuhubiri mazuri ya uislamu kwa kutoa ushuhuda wake kwamba aliacha kuwachukulia wazungu wote kama maadui, akasisitiza zaidi katika maisha yake yote hakuwahi kushuhudia ukarimu wa dhati na roho ya kweli ya udugu kama aliyokutana nayo Makka. Akahitimisha akaona dini ya uislamu inaweza kuwa mbadala ya kufuta ubaguzi wa rangi uliyopo Marekani. Alishuhudia maelfu ya watu wakiwa Makka wakishirikiana pamoja kwa kula pamoja, kunywa pamoja na kusikilizana. Na hilo likampa funzo kubwa ya kutowachukia wazungu maana alivyokuwa Makka alikutana na wazungu wenye roho nzuri na upendo lakini hii yote ilikuwa ni kwa sababu ya uislamu.
Mimi sijaenda Makka na siyo lazima kila mtu aende Makka ndio atende mambo mazuri ila hayo mazuri nimejifunza uswahilini kwetu ambapo huwa tunakutana kufanya ibada. Dunia ni mahala salama kama watu wakiongozwa na upendo wa dhati.
#mlimwengumimi
#ramadhankareem