Kikarara78
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 1,495
- 901
Nawaza Tu:
Nguvu ya imani juu ya unachokiamini. Nimekua nikifuatilia mojawapo ya mambo yanayoendelea na limenifanya nirudi kwenye maandiko kidogo. Wakati Shetani anataka kumuangamiza Ayubu Mungu aliruhusu achukue Wanae, Mali zake na Heshima yake yote kwa jamii. Mungu pia aliruhusu Shetani ampe magonjwa ambayo yalifanya Ayubu asiwe na afya njema aliyokua nayo kipindi ni Tajiri. Nguvu ya Imani juu ya anachokiamini ilishinda majaribu yote na mwishowe Mungu alimpa Ayubu mara 7 ya alichokua nacho mwanzoni. Storii hii inanifanya nimkumbuke Mzee Wetu Madiba aka Mandela alipokaa jela miaka 27 akiteswa na makaburu wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo wanambadili mawazo na kusaliti wenzie aliokua anawapigania..Hili nalo lilishindikana na Mzee Madiba akawa Rais na watu wale wale wakampigia saluti.
Ni nguvu ya Imani mtu anayokua nayo juu ya kitu anachokiamini. Mifano ni mingi ambapo watu walipopelekwa magerezani waliweza kuandika Best selling movies,Best selling novels na waliweza kupata muda wa kujijenga kiimani zaidi na kuwa stronger kuliko walivyoingia jela.
Kibinadamu kumuweka mtu gerezani pamoja na kumfilisi mtu mali tunadhani ni silaha ya kumdhoofisha. Historia inatufundisha kuwa Nguvu ya Imani hushinda 'majaribu' yote na Mtu huinuliwa kwenye level nyingine tofauti na alipokuwepo mwanzoni.
Mali, heshima ,watoto,mke au Mume ni vitu ambavyo huwa tunapewa na muda wowote huweza kuchukuliwa .Imani zetu zinaweza kuwa challenged muda wowote kama Ayubu na kama huna Nguvu inayohitajika ni rahisi kusaliti kile unachokiamini.
Magereza yamezoeleka kua ni sehemu za kudhoofisha watu lakini pia yameonyesha kua ni sehemu tulivu ya mtu kuongeza Nguvu ya imani.Kwa tuliopitia sunday school kuna kawimbo tulikua tunaimba, Pauloooo na Silaaaa waliombaaaa milango ya gereza ikafunguka*3.
Source: Mdau Mmoja FaceBook aka PanyaBook.