I'm looking for serious business patners

Ccreation

Senior Member
Sep 27, 2015
145
55
Wadau si mara ya kwanza kuingia hapa na kushawishi watu wenye nia ya kuungana katika biashara ,Mimi mbali ya biashara nyingine ndogondogo ninauza CEMENT .biashara hii ni kama unauza chakula kwa maana haiwezi kushindikana kuuzika , hadi mfuko wa mwisho.
FURSA YA KUPIGA HATUA:
baada ya kuanza nimepata kujifunza fursa kubwa ya kupiha hatua ya maendeleo kama watu mtakua na nidhamu ,KUNA faida itokanayo na kila mfuko kati ya 300 hadi 700 kulingana na aina ya CEMENT na gharama za uendeshaji, pili kuna bonasi kutoka kampuni husika, kwa mfano wanakuambia ukiuza tani 10000 wanalipa bonasi tsh100 per bag, (semi ya tani 30 mifuko 600 unaweza kuona hesabu ikoje,lakini pia kuna fursa ya kuanzisha biashara ya tofali hapa inalipa zaidi, nia yangu kubwa ni kushauri vijana wenzangu kuunganisha nguvu tukaanzisha kampuni moja yenye nguvu kubwa ya wapambanaji kukabili changamoto za mitaji,masoko na utawala.
Tukiungana tukahitaji milioni 100, kuna uhakika wa kupata kuliko kwa mtu mmoja kuzitafuta,
Watu huogopa kushirikiana lakini ni jambo zuri sna na mnaharakisha maendeleo, kwa mfano miongoni mwetu tunaweza kupata wataalamu mbalimbali ,wa fani tofauti na kufanya mtaji wa kwanza ni taaluma za wanachama,

Malengo ya baadae ni kuwa na kampuni kubwa ya UJENZI , Haya yanawezekana ,ndoto zinaweza kuwa kweli

KWA YEYOTE MWENYE KUVUTIWA NA MPANGO HUU:
TUWASILIANE ,0762576878,

Milioni 100 kwa watu 50 ni milioni 2 kila mmoja ,shuka na hesabu hiyo mpaka utakapoona inafaa kwa idadi ya wanachama ambao ungependa wawepo na kiasi cha kuchangia

Baada ya kuwa pamoja tutatengeneza uhusiano mzuri na mabenki ,ambapo tunaweza kupata mikopo au bank gurrentee,

Kama kuna MTU anasoko tu LA cement anaweza kuwa mkombozi mkubwa maana biashara ni soko,hivyo kuwa wengi kuna faida zake,

Maelezo hayana mpangilio mzuri sana lakini nadhani ujumbe umeelweka ,karibuni
 
Hili wazo ni zuri sana sema changamoto huwa inakuwepo kwenye uaminifu wa sisi wa tz
 
Hujaeleza milioni 100 mpango wake na faida unayotegemea. Au visibility study yake tueleze
 
100 milioni itatumika hv, :tani 30 ya cement ni sawa na mifuko 600, ambayo ni semitrailer 1= tsh 6,000,000/=bila ya gharama ya usafiri na kushusha, hivyo tunaweza kununua tani tani 450 ambayo ni sawa na semi 15, mifuko 3000 ya cement, kwa gharama ya mil 90 , na tutabakiwa na mil 10 kama salio la kugharamia ,usafiri na mengineyo, tukiuza cement ya dangote kama super dealers hakutakuwa na gharama za usafiri, kwa kutumia wingi wetu tutajipa jukumu la kutafuta soko, mbali ya mpango kazi wa kuendesha biashara ,( Ununuzi na mauzo)mfuko mmoja wa cement unauzwa 10000 na kuuzwa 11500 jumla na 12500- 13500 rejareja sasa tukiweza kuuza tani 60 kwasiku na kupata faida ya wastani wa tsh 1000 kwa mfuko basi mtaweza kuuza tani 1800 kwa mwezi sawa na mifuko 36000 , na faida ya 36,000,000/= ktk mwezi mmoja , na ndani ya mwaka ni tsh ni mil 432, inaweza kupungua ukitoa gharama za kodi na uendeshaji , JE UKIWA PEKE YAKO UNAWEZA KUTENGENEZA TSH NGAPI KWA MWAKA KWA MTAJI WA MIL 2? TAFAKARI
 
Wazo zuri sana, nimekuwa interested ila nashauri tuzame kwenye soko la chuma like squre pipes na flatbars,

Mimi niko huko tayari ukiwa interested let us join kama shareholders.
 
Kazi Sana kibongobongo kuunganisha watu kuwa "same thinking" ndani ya hao watu utawapata
1.wanapenda ngono
2.walevi na vibaka
3.wavivu
 
Back
Top Bottom