Ilinitokea maeneo ya Morogoro sina uhakika kama ni sahihi - Tujadili

monomotapa

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
437
325
Nilikuwa na familia yangu nasafiri na gari binafsi kuelekea mikoa ya nyanda za juu kusini nilipofika maeneo ya Kingorwila Morogoro kuna kituo cha polisi nakifahamu vizuri sana kipo kandokando ya barabara kuu na kuna matuta pia eneo hilo. Nilipita pale nikiwa na mwendo wa 30 mpaka 40 nikifahamu wazi kuwa ni kisehemu kina watu wengi na ni kamji kadogo hivi na pia pana malekezo ya 50KM. Baada ya hapo kama mwendo wa dkd 6 hivi mbele kulikuwa na foleni hivi mbele nadhani madereva wanafahamu wapi traffic wapo hivyo nami nikawa katika mlolongo huo wa kwenda taratibu maana 50 kmh ilikuwa haijakatwa.
Cha kushangaza mbeleni kidogo nilisimamishwa na traffic tukiwa kwenye hiyo foleni na akanisalimia vyema sana na kwa nidhamu nzuri kabisa ( Ni kama mtoto wangu kiumri) Akanambia anaomba leseni nikampatia then alipochukua akanambia Mzee ulikuwa unaenda mwendo wa kasi eneo la Kingorwila, nilipigwa na butwaa na kumuuliza kama anafanisha magari..Then akanambia ninaweza kurudi mpaka kingorwila kama nataka kujiridhisha ila picha imetumwa (Yeye alisema wamerushiwa) inasemekana ilikuwa kwenye simu ya trafic mwingine (WP) Nilienda kuangalia nikiwa nimetaharuki ila niliweza kuji control nikaonyeshwa picha nikawaambia hii si gari yangu, huyo WP alionekana pia kama ana wasiwasi akapekua akanionyesha picha nyingine nikaangalia ile picha imepigwa kwa nyuma na gari inataka kufanana na yangu ila sikutakata kubishana nao kwasababu nawaheshimu sana polisi na pia kulikuwa nakajua ka kali hivi nje. Nikamwonyesha Madam wangu pia hakuelewa kwasababu tulikuwa tunakwenda below 50kmh yeye pia ni dereva kama mimi na tunakumbushana kuhusu alama za barabarani wakati wote....Kwakuwa kulikuwa na mwanga wa jua na simu yenyewe haionyeshi vyema na pia sikutaka kuweka ligi nao nikawaambia sidhani kama tunaweza kuunguza mafuta na kupoteza muda kurudi huko Kingorwila. Wakanambia niwalipe faini ya TShs 30,000 /= nikawapa nikawataka watumie EFD wakanambia hawana ila naweza fuahatilia pale Msamvu kuna trafic anayo mashine hiyo (Maelekezo yao) Anyway nililipa kwa utaratibu wao wa zamani (Nikaamua niachane na kuanza kazi ya kufuatilia EFD huko Msamvu)
Wakati tumeamua kuendelea na safari tukawa tunatafakari maana 30,000 sio hela ndogo kuitoa kirahisirahisi hivi, tukagundua tulikuwa tunahitaji kufahamu zaidi mambo yafuahatayo:
1. Picha inaonyesha gari limepigwa kwa nyuma peke yake na ndo imejaa kwenye screen yote ya simu, haionyeshi mazingira imepigwa eneo lipi ili kujiridhisha kuwa ni eneo halali dereva anatuhumiwa kuvunja sheria ya barabara ( Uwezekano wa kubambikiwa upo)
2. Namba ya gari haionekani vizuri ni kama picha imecheza hivi ila waweza tambua kuwa hii ni aina fulani ya gari ingawa inaweza kuwa si yako (Magari yanafanana) - Ingawa picha imeambatana na speed iliyo zaidi ya 50 ikiwa na maandishi mekundu
3. Trafiki kurushiana picha ni sawa katika sheria za usalama barabarani?
Wenye utaalamu ama experience ya matukio kama hili ama zaidi tunaweza zileta hapa tujadili, - Lugha isiwe kavu sana (Hapana matusi ama mambo ya vyama) hii ni kitu muhimu na inatugusa wote kabisa maana kusafiri hakuepukiki - Natanguliza shukrani
 
Wanachofanya traffic kwa sasa ni kuweka watu wakupiga picha mfano pale kwenye kibao cha Jordan university college Moro kuna mdada Na mkaka wamekaa kazi yao ndo hyo kupiga picha Na kurusha kwa matrafic hivyo yawezekana picha haijapigwa Kingolwira...
 
Wanachofanya traffic kwa sasa ni kuweka watu wakupiga picha mfano pale kwenye kibao cha Jordan university college Moro kuna mdada Na mkaka wamekaa kazi yao ndo hyo kupiga picha Na kurusha kwa matrafic hivyo yawezekana picha haijapigwa Kingolwira...
Aksante kwa kunielewesha , sasa hiyo university ipo eneo gani? Ni mbele ya kingolwira ama ni kule nyuma kwenye mikonge?
 
Kwa sasa faini ndo zinaonekana kuwa tegemeo la pato la taifa. Lazima wakomae
 
Kiukweli ilikuwa ni vema kama no ya gari ingeonekana pamoja na mazingira kwa kuwa magari mengi sana yanafanana
 
Ndo zao hao skuiz,wamekuwa wahuni sana.mimi safari ndefu kama hizo huwa najitahidi kuongozana na mabasi makubwa maaana ndo wanawajulia vizuri
 
Back
Top Bottom