Ilimu ya tanzania haifikii malengo yake. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ilimu ya tanzania haifikii malengo yake.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by NGOWILE, Oct 28, 2011.

 1. N

  NGOWILE JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 454
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Lengo kubwa la elimu ni kumuandaa mtu ili aweze kukabiliana na mazingira yanayomzunguka.Si lengo la elimu mtu kuzunguka na vyeti kutafuta kazi za ofisini tu.Katika fikra za MWALIMU alisema elimu ya Tanzania ni lazima imuandae mtanzania ili aweze kujitegemea mwenyewe ikiwa ni pamoja uwezo wa kuwa na fikra sahihi pamoja maamuzi sahihi(mambo sahihi hutokana na fikra sahihi)
  -Asilimia kubwa ya walimu wa Tanzania wamekuwa walimu baada kukosa nafasi kwenye taaluma nyingine.
  -Wanafunzi wengi wa shule za msingi wanakaa chini na wengine chini ya miti.
  -Walimu wachache waliopo hawana maslahi ya kutosha hivyo wamekata tamaa.
  -Asilimia kubwa ya walimu ni wale waliofaulu viwango wa chini sana kwenye elimu ya sekondari.
  -Idadi kubwa ya wanafunzi darasani kuliko uwezo wa darasa.
  -Shule kukosa nyumba za walimu.
  -Kutokuwa na bodi ya walimu.
  -Mtihani shule za msingi kuwa na maswali ya kuchagua tu(multiple choice) mpake hesabu.
  KWA KUZINGATIA NILIYOYATAJA,LENGO LA ELIMU TANZANIA LINAFIKIWA?
   
Loading...