enockino
JF-Expert Member
- Oct 14, 2014
- 273
- 171
Imeelezwa kuwa kabla ya kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya tano, ilikuwa ni aibu kwa watanzania wanaokuwa nje ya nchi kujitambulisha kuwa ni watanzania kutokana na mambo ya aibu yaliyokuwa yakifanyika nchini.
Hayo yamebainishwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Dkt. Abednego Keshomshahara katika salamu zake za ibada ya Krismasi kitaifa iliyofanyika Mjini Bukoba leo, ambapo amesema tangu kuingia kwa serikali ya awamu ya tano, hali ni tofauti, na kwamba kwa sasa Tanzania inasifiwa kila kona
Dkt. Abednego ametaja jambo kuu la aibu lililochafua sifa ya Tanzania katika jumuiya ya kimataifa kuwa ni mauaji ya albino yaliyokuwa yameshamiri hasa mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo mkoa wa Kagera pamoja na vitendo vya rushwa na ufisadi hali iliyokuwa imefanya sura ya Tanzania iwe chafu kiasi cha watanzania kuona aibu kuitangaza nchi yao.
"Wakati ule nikiwa nje ya nchi ilikuwa aibu kujiita Mtanzania kwa sababu mauaji ya albino yalikuwa yameichafua nchi sana, lakini kwa sasa mauaji yanakwenda yanaisha kutokana na kuimarishwa kwa ulinzi pamoja na mahubiri ya viongozi wa dini na niwaambie ukweli tunasifiwa sana huko nje" Amesema.
Ameipongeza serikali kwa kudhibiti vitendo vya rushwa na ufisadi pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara, kutoa elimu bure, kuweka mazingira mazuri kwa dini mbalimbali kuendesha shughuli zao, kukarabati miundombinu ya umma iliyathiriwa na tetemeko la ardhi huku akiiomba kuendelea kusadia wasiojiweza katika tetemeko hilo na ikiwezekana kuwasaidia kujenga.