Ilikuwa hivi akakataa kura

Kabewa

Senior Member
Oct 30, 2009
136
56
Mie ndiye muajiri mkuu nisikilizeni mimi, msimsikilize Mgaya (Kaimu Katibu
Mkuu TUCTA) mtafukuzwa kazi wala Mgaya hamtamuona! Mtapoteza haki zenu…akili ni
nywele kila mtu ana zake mtu mzima dawa," alisema Kikwete ambaye alikuwa
akishangiliwa na wazee hao.

"Sasa hata hatujazungumza wameanza kutangaza mgomo, sasa afadhali tuzungumze
kwanza maana mgomo una kasheshe zake, mkigoma hamtaachwa, askari watawapiga
virungu na hata wengine kuweza kupoteza maisha, mimi naweza kuwa rahim (mwenye
huruma) lakini polisi mkiwafanyia fujo watawatwanga na hata mkigoma baadaye
mtarudi kwenye mazungumzo mkiwa na plasta midomoni,"alisema na kushangiliwa na
wazee hao waliokuwa wakitoa maneno kuwa wamechoka (wafanyakazi) waende wakalime
mpunga.

"Kama hawataki wasinipigie kura…nitazipata kwa wengine ambao wanataka
kudhulumiwa na hawa wafanyakazi…kwa sababu fedha za serikali ni kwa ajili ya
Watanzania wote milioni 39 sasa hizi trilioni sita zinahitajika kwenda kununua
madawa, ruzuku ya mbolea, maji, shule, umeme, barabara kwa faida ya kila mmoja
sasa kwanini ziende kwa wafanyakazi? Hii si haki ni madai yasiyo na msingi wa
haki," alisema na kuwafanya wazee wamshangilie huku wakiimba,

SWALI. JE WAFANYAKAZI TUKISEMA TUSIMPE KURA JK KWASABABU TU ALIKATAAKURA ZENU KAMA MNATAKA KUDHULUMU HAKI ZA RAIA WENGINE WASIO WAFANYA KAZI JE NA HAO WASIO WAFANYAKAZI AMBAO JK ALIWATETEA WOTE WAMPE KURA JK? ILI HALI ALIWATETEA DHIDI YA DHULUMA ZA WAFANYAKAZI?
 
Tatizo hajui kuwa hata madereva wake, walinzi, wapishi na wengineo ni sehemu ya hao wafanyakazi wake......akili bwana
 
Back
Top Bottom