Ilikufia wapi Tanzania house bank (THB)

aka2030

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
2,677
Reaction score
3,755
Jamani hili shirika lilikufaje wadau maana muda huu ndio lingekuwa mkombozi
 
Hilo nalo swali ndg yangu kwamba account i.iishia wapi, benki ikifilisika wateja si wanapewa chao ndg.

Miaka ya mwanzo ya 90, Wazazi walikua na vision nzuri na mimi ndg aka2030
 
Last edited by a moderator:
Lukuvi hebu onyesha jitihada
 
Mimi mwaka 1987 dingi alinifungulia account, nikiwa na miaka kama 11 hivi, nilikuwa naweka weka vipesa hapo baada ya kuwa nauza malimao, mwisho wa siku nikashangaa benki haipo bali jengo hilo sasa ivi ni TRA.
 
Ulikuwa Ta nini, maana jengo la THB ni la TRA kwa sasa.
 
Liliibiwa watu wakanywa kama yalivyokufa mashirika ya umma karibia yote.
 
Wakubwa wengi walikopa huko. Wanaona bora waiue kimya kimya maana orodha ingetoka, ingekuwa aibu. Tusiowadhania walikuwemo kama wadaiwa sugu.
 
Wakubwa wengi walikopa huko. Wanaona bora waiue kimya kimya maana orodha ingetoka, ingekuwa aibu. Tusiowadhania walikuwemo kama wadaiwa sugu.
Biashara ya benki ni kukopesha. Tatizo wezi.

Tanzania hakuna shirika la umma litasalimika, labda tuanzishe sheria za kuuwana.
 
Yupo mzee mmoja Urasa ndio alikuwa mkurugenzi mkuu was hiyo benki.

Yuko vizuri Sana nadhani mchwa waliitafuna THB. Ingesaidia Sana tatizo la housing estates tungekutana Kama Kenya. Well surveyed and planned settlement.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…