Ilikua balaa.

Muuza Viat

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2022
Posts
2,881
Reaction score
7,495
Km kawaida yangu nilikua ndani ya soko la karume mchikichin napiga mishe zangu za usabanga ili nipate rizki ya kuweza kumudu matumizi yangu ghafla tambo likaita kuangalia mpigaji namba ngeni Mzee mzima nikapokea na kumsikiliza mpigaji



Mpigaji alijitambulisha kuwa ni askari polisi kutoka kituo cha sentro na alinitaka siku inayofata mida ya saa nne kamili usubui nihudhurie kituon bila kukosa


Baada ya kumaliza maongezi nikawashirikisha wadau nilichokiongea na yule aliyejitambulisha kuwa ni askari wadau wakanishauri kuwa wew nenda kasikilize wito


Huwezi amini siku ilifika na muda ukafika na km kawaida yetu waswahili nilikaa sokoni mpaka saa tano kasoro ndio nikaanza safari ya kwenda kituon


Baada ya kufika kituon nilienda moja kwa moja mapokezi na kumuulizia yule afande niliambiwa ametoka km vp nimcheki hewan na baada ya kumpigia alinijibu nimsubiri ndani ya nusu saa atakuwa ameshafika


Baada ya jibu lile nilitoka nje ya kituo na kufanya tathmini kuwa kwa nini nikae pale nusu saa nzima nimsubiri ilhali mimi mwenyewe nina mambo kibao ya kufanya na ukizingatia hiyo nusu saa aliyoahidi inaweza kufika hata zaidi ya saa mwishowe niliona bora niondoke na km akifika akinipigia nitachukua boda fasta na kuja pale kituoni


Mzee mzima nikaanza safari mdogomdogo mpaka pale trafiki nikavuka barabara mpaka treni ya mwendokasi ghafla tambo likaanza kuita naangalia namba ni ngeni tena imepigwa kwenye laini ambayo huwa siitumii kwenye kupiga wala kupigiwa ni laini niliisajili kwa ajili ya kuweka pesa tu sikushtuka niliona kuna mtu amekosea namba ngoja nipokee nimfahamishe kuwa kakosea


Baada ya kupokea kumbe alikua yule yule afande na kitendo cha kusikia sauti yake tena kwenye namba ambayo mwenyewe naitumia km bonye kilinichangànya,alianza kwa kuniuliza unaenda wapi? mzee mzima nikajikuta naàngalia pande zote,akaendelea kuniambia kuwa bràzà kwa heshmà nimekupigia simu nà kukwàmbia uje kituon lkn nilikua na uwezo wa kukufata kinomanoma nà difenda miksa kufungana pingu lkn hayo yote mimi sikuyataka lkn wewe unaniona mimi fala
Nilikwambia ufike kituon saa nne lkn wewe ulifika saa tano na nilikwambia unisubiri lkn wewe hapo ulipo unaondoka sasa ww nenda na naamini hutonilaumu


Dooo! Mzee mzima baada ya ile simu kukata nikajikuta nimetoka mbio Usain bolt anasubir mpaka pale kituoni na ilibidi niulize yule askari anashughulika na nini jamaa wakanijibu anashughulika na makosa ya mtandaoni hapo ndio wakanivuruga kabisa


Ilibidi nianze kufatilia komenti zangu mitandaon nione labda km kuna sehemu nilizingua lkn nilikosa jibu mwishowe niliona ngoja niangalie ghàrama za kumkodi wakili kibatàla huku napo nilikwama


Mungu na wanadamu yule askari alifika akaniita ofisiñi kwao mule ndani na jambo la mwanzo kuniambia weka simu ubaoni na baada ya kuiweka aliniuliza uliipataje hii simu


Ile simu niliinunua kkoo baada ya kuinunua nilichukua risiti,simu na chaja boks nililiacha pale pale,watoto wa mjini walichukua boks likiwa na makaratas yote yanayoihusu simu yangu wakaweka simu iliyotumika na kumuuzia mtu mwingine na yule mtu hakumaliza hata wiki tambo lake likaibiwa kwa hiyo yule mtu alichokifanya alibeba boks na makaratas yote pàmoja na risiti mpaka police
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…