Elisha Chuma
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 282
- 275
Tatizo kubwa la kushindwa kunyanyuka ni mentality yako ina nguvu kiasi gani na uwezo wa kuchambua na kutafuta chanzo kwanini umeanguka wengi tukianguka haturudi kwenye liliotuangusha tunaliacha tunatafuta jipya wakati lililokufanya ukaanguka limekufunza,unaenda kwenye jipya nalo linakuangusha unaacha mwisho wa siku muda na nguvu havikusubiri...unalaumu kila kitu na kusema kwako havifanikiwi.Ule uwezo wa kunyanyuka baada ya kufeli, ndiyo mwanzo wa mafanikio.
Chukua ukajengee.Mr Posibility said:Nondo hii
Tunahitaji sana kubadilisha fahamu za vizazi vyetu ili kutengeneza uchumi tunaoufikiria...wengi wanafeli sio kwa kukosa uwezo ila ufahamu mdogo na dhana zenye mihemukoKufanikiwa ni kutatua changamoto au kusolve tatizo linalokusibu. Na ili ujue tatizo, anza kwanza then ukikosea unalirekebisha. HAPO NDO UMESHAFANIKIWA!
Kwa mantiki hyo, NAUNGA MKONO HOJA!
Wengi wakianguka wanaacha kwa sababu hawakuwahi hata kujipima kwa jambo hilo tunafanya biashara za kujaribu kama italipa ndio maana ikikupa changamoto unaikimbia japo kuna wengine uliowaona ukawatamani wanafanya hiyo hiyo na maisha yanaendelea.Thts a very big mistake!.ukishaweza kusimamia jambo moja ukianguka hata mara7siku ukinyanyuka umenyanyuka
Ha ha ha haaaaa......Chukua ukajengee.
Hapa kwenye kuzikimbia changamoto ndio shida ya wengi. Hivi unadhan ukizikimbia huku, kule unakoenda hakuna?Elisha Chuma said:Biashara za kujaribu kama inalipa ndio maana ikikupa changamoto unaikimbia
Food for thoughtSehemu kubwa ambayo bado kama taifa na mtu mmoja mmoja tunafeli sana ni kwenye eneo la ujenzi wa ufahamu kwa watoto na vijana,Asilimia kubwa ya fahamu zetu zimekariri ushindi sana kuliko hatua za ushindi.
Hii haiko kwenye biashara tu bali hata kwenye maisha yetu ya kawaida,mahusiano,uchumi na kila kitu.
Fahamu zimejengwa kila unachofanya tegemea kushinda tu,lakini pia hata washauri pia ama motivational speaker tumejikuta katika wimbi lile lile kuwaambia watu mbinu za ushindi tu lakini uhalisia wake ni kushindwa.
Hauwezi kujua kama umeshinda iwapo hujui kushindwa,hakuna safari isiyokuwa na vikwazo,ikikosa vikwazo inapunguza umuhimu wake,ndio hata maisha ni taratibu za kutatua changamoto siku baada ya siku na ukifanikiwa unaita ushindi na unapata furaha.
Mafanikio yanagharama yake na moja ya gharama ni vikwazo na kufeli ili upate thamani ya mafanikio halisi,hivyo katika kila unalolifanya tegemea kuna kufeli ama kufanikiwa hata kama ufahamu wako umeuelekeza kufaulu lakini jipange na ikitokea umefeli ili isikuvunje nguvu.
Leo hii wajasiriamali wengi wanafeli sokoni sababu walijiandaa kufaulu tu,ndoa nyingi zinavunjika sababu zilijiandaa furaha tu,mahusiano mengi hayadumu sababu yanataka raha tu.mikopo inakuwa shida marejesho sababu hakuna kujipanga na iwapo ikitokea nimekosa nitafanya nini, karibia kila kitu kinasababishwa na kutokujiandaa kwa matokeo hasi.
Badilisha mtazamo wako na fungua ufahamu wako,changamoto ndio ukuaji,changamoto unayoipata leo ndio itakayokuimarisha kesho.tatua na endelea jenga ufahamu vizuri kwa kizazi chako pia.
Ili ufanikiwe unahitaji kufeli ili uione gharama na hadhi ya kufikia mafanikio.
Elisha Chuma.
View attachment 1283694
Loser sio looser"WINNER is just a LOOSER who tried one more time"
japo kuna mda unaluzi mpaka sio poa yaan unagusa biashara hii, unapoteza laki 7 chap,unagusa ile unapoteza milion,unagusa nyingne unajikuta unazika mamilion daaah unakaaaa unatafakariiiii afu unajinyamazia anyway mwiko kukata tamma[emoji123]
Shukrani kwa mada bomba sana mkuu E. C.Sehemu kubwa ambayo bado kama taifa na mtu mmoja mmoja tunafeli sana ni kwenye eneo la ujenzi wa ufahamu kwa watoto na vijana,Asilimia kubwa ya fahamu zetu zimekariri ushindi sana kuliko hatua za ushindi.
Hii haiko kwenye biashara tu bali hata kwenye maisha yetu ya kawaida,mahusiano,uchumi na kila kitu.
Fahamu zimejengwa kila unachofanya tegemea kushinda tu,lakini pia hata washauri pia ama motivational speaker tumejikuta katika wimbi lile lile kuwaambia watu mbinu za ushindi tu lakini uhalisia wake ni kushindwa.
Hauwezi kujua kama umeshinda iwapo hujui kushindwa,hakuna safari isiyokuwa na vikwazo,ikikosa vikwazo inapunguza umuhimu wake,ndio hata maisha ni taratibu za kutatua changamoto siku baada ya siku na ukifanikiwa unaita ushindi na unapata furaha.
Mafanikio yanagharama yake na moja ya gharama ni vikwazo na kufeli ili upate thamani ya mafanikio halisi,hivyo katika kila unalolifanya tegemea kuna kufeli ama kufanikiwa hata kama ufahamu wako umeuelekeza kufaulu lakini jipange na ikitokea umefeli ili isikuvunje nguvu.
Leo hii wajasiriamali wengi wanafeli sokoni sababu walijiandaa kufaulu tu,ndoa nyingi zinavunjika sababu zilijiandaa furaha tu,mahusiano mengi hayadumu sababu yanataka raha tu.mikopo inakuwa shida marejesho sababu hakuna kujipanga na iwapo ikitokea nimekosa nitafanya nini, karibia kila kitu kinasababishwa na kutokujiandaa kwa matokeo hasi.
Badilisha mtazamo wako na fungua ufahamu wako,changamoto ndio ukuaji,changamoto unayoipata leo ndio itakayokuimarisha kesho.tatua na endelea jenga ufahamu vizuri kwa kizazi chako pia.
Ili ufanikiwe unahitaji kufeli ili uione gharama na hadhi ya kufikia mafanikio.
Elisha Chuma.
View attachment 1283694
shda yako ni grammar yangu au idea nlotaka ku present hapaLoser sio looser