Ili tusiyumbishwe na ili tusimamie misimamo yetu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,694
149,917
Ili usiyumbe na zaidi ili uwe na msimano katika kile unachokiamini, achana na kuangalia majina ya watu, ID zao,umaarifu wao au misimamo yao ya siku za nyuma na ikiwezekana soma content ya mada yake kwanza uipime na jina/ID yake uisome mwishoni kabisa.

Hawa watu ni binadamu kama sisi na wanaweza kuwa na interest zao na wanaweza kubadilika wakati wowote kutokana na sababu mbalimbali na sababu hizo zinaweza kuwa ni kutokana na ugomvi binafsi,chuki binafsi,maslahi binafsi,n.k.

Humu ndani hatujuani na hivyo huwezi jua mtu kagombana na nani, kagombana na kiongozi wa chama gani,kama kafukuzwa uanachama yeye mwenyewe au mke wake,n.k na hivyo akaanza kubadika katika misimamo yake na wewe bila kutafakari wala kujiuliza unaanza kupata tabu juu ya msimamo wake mpya au kubadilika kwake.

Wewe kama ni mfuasi wa chama fulani au kiongozi fulani always simamia principal zako na mtu akikushawishi ubadili mtizamo wako basi afanye hivyo kwa
kukushawishi kwa hoja ila si kwa ID yake/jina lake tofauti na hapo utapata shida sana.

Tuwe great thinkers na sio great followers.

Ikiwezekana uongozi wa JamiiForums uanzishe Jukwaa maalumu la semina juu ya matumizi bora ya mtandao na watafute wataalamu wa kutoa semina.
 
Back
Top Bottom