Ili Nape aendelee kuilinda heshima yake, ahame CCM.

H.T.P

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,169
1,298
Kama tukiongea ukweli bila unafiki wowote, Mh Nape hapaswi tena kuwa CCM kwasababu:

Kwanza; amedharauliwa mno! Magufuli ndo mwenyekiti, na kitendo cha kumtengua Nape kibabe namna ile ni dharau kubwa na kejeli; inamaanisha, Nape hana thamani kwake hata asipokuwepo. Nape unasubiri nini?

Pili; Nape mchango wake hauna umuhimu kwa CCM, Nape kipindi cha kampeni alitumia kila aina ya silaha hata ikiwa kumtukana MTU ilimradi ushindi upatikane, lakini wakamtafuna kama Big G sasa wamemtema. Nape unasubiri nini?

Alex Furgerson aliondoka Man U wakiwa bado wanamuhitaji ili kulinda heshima yake ambayo aliona, akiendelea kubaki, ingeshuka kama ambavyo tunamuona mzee wetu mpendwa Wenger. Nape unasubiri nini?

Akumulikaye mchana, usiku anakuchoma. Nape we ni mwana CCM unaujua uhuni na usanii Wa hiki chama, wanakupenda siku wanakuhitaji zaidi ya hapo we kwao ni Big G tu. Nape unasubiri nini?

Siumeona baada ya kuona mwenyekiti anaharibu akaamua kumpa mama Salma ubunge, ili aongeze nguvu kwenye kampeni zijazo, lakini asingeharibu, mama hata ujumbe tu kwenye chama sijui kama angepata.

Kuna mengi ya kuuambia nape lkn ngoja kwanza niwaachie wengine nao wanasemaje. Ila mi nasema kahesima kaliko baki katunze kwa kuhama kuliko kufukuzwa, hawa watu hawana maini eti.
 
nililitegemea hili...watu watahakikisha wanakuharibia huku wakicheka na wewe...nape kama anataka kujua wabaya na wazuri wake ahame CCM... as m very sure akisha lost watamkimbia wooote... Akili kichwani kwake ndugu yetu huyu..
 
Kuna wakati tunajadili sana siasa kuliko maisha yetu na Tanzania yetu kesho tutakapo letewa kuwa mbuga za wanyama hamna wanyama tutaanza kumlaumu raisi kumbe sisi tunasahau kufuatilia rasilimali zetu. Tunafuatilia rasilimali za ccm ambazo hajiwezi kuja kutusaidia nape ni rasilimali mhimu kwa ccm ila ni mzigo kwa upinzani atakapo hamia upinzani atakuwa rasilimali wa upinzani
 
Nape, kama ana busara akae kimya na wala asihame CCM. Kelele za wapinzani na waandishi wa habari hazitamsaidia chochote. Umaarufu alionao aliopata kwa sababu ya CCM. Akihama atakuwa hajatumia busara. Awaulize wenzake waliohama wama achieve nini tangu wahame ndo ataelewa. Kuna watu wanafurahi yaliyomtokea Nape. Kikubwa asifanye jambo kuwafurahisha watu, atapotea
 
Nape ni mtu mzima, anamaamuzi yake binafsi, na vile vile mtu anaejitambua husimamia kile anachokiamini, sio busara kufanya maamuzi yoyote ukiwa katka hali ya hasira au uchungu.
 
yeye na Bashe (Mod sijasema Bash.it.te.sina M5) wakae huko wawanyooshe Kijani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom