N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 6,825
- 9,533
Itakuwa vema ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa maeneo muhimu ya mjini kv eneo la makaburi ya sinza, Kinondoni, makaburi ya mabatini mwanza, makaburi ya askari wa kale nk.
Nashauri siku za usoni tufanye hivyo kwa kufukua makaburi yote maeneo ya katikati ya miji ambayo yanafaa kwa uendelezaji kisha hiyo miili tuihifadhi katika makaburi ya chini ya Ardhi/mahandkini.
Huko Paris Ufaransa kama unavyoona hapo pichani wenzetu wametunza mabaki ya miili ya marehemu kwa mtindo huo murua kabisa kiasi kwamba hakuna tena shida ya kubana maeneo ya uzalishaji kwa kuweka makaburi meeengi kama tunavyofanya sie.
Nashauri tuchukue haka kautaratibu.
Kaburi hili la pamoja unaloliona pichani limehifadhi mabaki ya marehemu zaidi ya Milioni Sita katika eneo dogo tu la handaki kwa mpangilio mujarabu kabisa………...Utaratibu huu ulibuniwa miaka ya 1774 kutokana na maeneo ya miji kutopatikana kwa maeneo ya maziko.
Hapa kwetu tumefikia hatua hatuna maeneo ya kuzikia...hivi leo watu wanangángániana maeneo ya kuzikia hata kufikia kufukua miili au kuzika juu ya makaburi ya wengine. Tuchukue haka kautaratibu.
Tangu wafaransa wabuni mtindo huu ambao pia umeigwa huko Italia ndugu jamaa na marafiki wamekuwa wakipeleka mabaki ya marehemu wao kwenye eneo hili.
CC: Wanabodi wote
CC: Mshana
BCC: Secretary wa Nyadikwa