Ili kuweka matumizi sahihi ya maeneo kwenye miji yetu makaburi yote yakiondolewa kisha tutengeneze catacombs kama Paris au Italia

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,530
2,000
Itakuwa vema ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa maeneo muhimu ya mjini kv eneo la makaburi ya sinza, Kinondoni, makaburi ya mabatini mwanza, makaburi ya askari wa kale nk.

Nashauri siku za usoni tufanye hivyo kwa kufukua makaburi yote maeneo ya katikati ya miji ambayo yanafaa kwa uendelezaji kisha hiyo miili tuihifadhi katika makaburi ya chini ya Ardhi/mahandkini.

Huko Paris Ufaransa kama unavyoona hapo pichani wenzetu wametunza mabaki ya miili ya marehemu kwa mtindo huo murua kabisa kiasi kwamba hakuna tena shida ya kubana maeneo ya uzalishaji kwa kuweka makaburi meeengi kama tunavyofanya sie.

Nashauri tuchukue haka kautaratibu.Kaburi hili la pamoja unaloliona pichani limehifadhi mabaki ya marehemu zaidi ya Milioni Sita katika eneo dogo tu la handaki kwa mpangilio mujarabu kabisa………...Utaratibu huu ulibuniwa miaka ya 1774 kutokana na maeneo ya miji kutopatikana kwa maeneo ya maziko.

Hapa kwetu tumefikia hatua hatuna maeneo ya kuzikia...hivi leo watu wanangángániana maeneo ya kuzikia hata kufikia kufukua miili au kuzika juu ya makaburi ya wengine. Tuchukue haka kautaratibu.

Tangu wafaransa wabuni mtindo huu ambao pia umeigwa huko Italia ndugu jamaa na marafiki wamekuwa wakipeleka mabaki ya marehemu wao kwenye eneo hili.

CC: Wanabodi wote
CC: Mshana
BCC: Secretary wa Nyadikwa
arranged-skulls.jpg
32.jpg
b6d19f43cb234cb4b899b60927b4cb33.jpg
 
Tifubaby

Senior Member
Jan 19, 2018
182
500
Mwili wa ndugui aliyekufa unakusaidie wewe. Tunahitaji kuchukua tahadhari na ardhi yetu. Tunazika hovyo sana. Kuna kila sababu ya kuchukua hatua ili kunusuru maeneo ya uzalishaji.
Yaani ww mbona unakuwa kama hazikutoshi kaburi ni kumbukumbu kila mmoja na mila zake usitufanye tuwe mabuda tuchomane moto tubaki namajivu nyumbani tunafata mila zetu serikali ikihitaji eneo la makaburi wanatoa commision kwa ndugu na jamaa na wanatenga eneo raia wahamishe miili ya ndugu zao sehemu walizo pangiwa siio hivo unavotaka wewe.
 
N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,530
2,000
Sasa hapo utajuaje mwili wa ndugu yako??

B.T.W Tanzania bado ni kubwa hatujawa na uhaba wa ardhi namna hio ni swala la planning nzuri tu mambo yanakaa poa
Ni kweli ila kwa miji kama Dar es salaam kwa sasa maeneo ya kuzikia hasa katikati ya mji imekuwa shida...kwa mfano sasa hivi mtu unatakiwa ukazike Tegeta huko maana Kinondoni pamejaa na huko tuendako miji kama Dar itakuwa issue sana kupata pahala pa kuzika.
 
N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,530
2,000
Mwili wa ndugui aliyekufa unakusaidie wewe. Tunahitaji kuchukua tahadhari na ardhi yetu. Tunazika hovyo sana. Kuna kila sababu ya kuchukua hatua ili kunusuru maeneo ya uzalishaji.
Hivi karibuni nilikuwa eneo la Bunju Beach natafuta plot nilishangaa kuona eneo la wazi kubwa tu limeachwa brokers wakaniambia hapo pana makaburi kama 20 tu na eneo la karibia sq m 1800 lipo wazi...ila serikali ya mtaa wamezuia watu wasiendelee kuzika hapo na badala yake waondoe makaburi ili eneo hilo litumike kwa shughuli nyingine za kijamii.
 
Kazakh destroyer

JF-Expert Member
Nov 16, 2017
907
1,000
kuzika ni ibada kwa waislamu kama ibada nyinginezo.....na maziko yana taratibu maalum wala si suala la kubuni na kujitungia tu,kama wanavyofanya watu wengine wanaenda na wakati utawaona hadi kwenye maziko teknolojia inakua....japo baadhi ya waislamu nao wanajengea makaburi na wameuacha muongozo wao wa asli ulioharamisha kabisa kuyajengea makaburi lengo kuu hasa ni kuiacha ardhi ikiwa haina alama isiyotoweka kiurahisi....kwa maana mtu anazikwa baada ya miaka 50-60 kaburi linakuwa flat na linatoweka kizazi cha wakati huo kinatumia maeneo hayohayo kufanya maziko na ardhi inabaki katika utaratibu wa kueleweka....bali katika uislamu wa sahihi ni ibada na ina utaratibu wake tangu zama hizo za kale na wala haubadiliki utaratibu huo mpaka qiyamah...kwahyo kaka ny'adikwa mambo mengine kwa kuhusisha imani za watu ni vigumu kuyatekeleza....
asante...
 
N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,530
2,000
kuzika ni ibada kwa waislamu kama ibada nyinginezo.....na maziko yana taratibu maalum wala si suala la kubuni na kujitungia tu,kama wanavyofanya watu wengine wanaenda na wakati utawaona hadi kwenye maziko teknolojia inakua....bali kwenye uislamu ni ibada na ina utaratibu wake tangu zama hizo za kale na wala haubadiliki utaratibu huo mpaka qiyamah...kwahyo kaka ny'adikwa mambo mengine kwa kuhusisha imani za watu ni vigumu kuyatekeleza....
asante...
Ni kweli ndugu wakati nikiliandika hili nilitafakari kwamba suala la Imani linakaaje ikiwa utaratibu huu unaweza kukubaliwa...lakini pia nikajiuliza kinachotunzwa humo ni mifupa mikavu ina maana kuna muda wa kusubiri...au wanafukua mabaki ya miili na sio kuzika moja kwa moja kwenye handaki husika..., ila nikaleta hoja jukwaani kama unavyojua hapa tunapata muono wa mawazo tofauti tofauti kuona linalowezekana...naamini sijakukwaza mkuu na kama nimekukwaza nisamehe bure haikuwa nia yangu. Naheshimu sana Imani.
 
busha

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
1,669
2,000
Ni wazo pia
Ila bado hatuja fikia kiwango hicho cha kukubali aina hii ya uzikaji kiimani na hata kimila
 
N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,530
2,000
DU humo ndani kutakua na mzimu hatari ukiingia humo lazima uyavagae
Kifinga watu wanaenda kutalii kabisa huko na handaki limekuwa ni kivutio cha utalii serikali inaingiza mapato kupitia mabaki ya raia wake wa zamani
 
Kazakh destroyer

JF-Expert Member
Nov 16, 2017
907
1,000
Ni kweli ndugu wakati nikiliandika hili nilitafakari kwamba suala la Imani linakaaje ikiwa utaratibu huu unaweza kukubaliwa...lakini pia nikajiuliza kinachotunzwa humo ni mifupa mikavu ina maana kuna muda wa kusubiri...au wanafukua mabaki ya miili na sio kuzika moja kwa moja kwenye handaki husika..., ila nikaleta hoja jukwaani kama unavyojua hapa tunapata muono wa mawazo tofauti tofauti kuona linalowezekana...naamini sijakukwaza mkuu na kama nimekukwaza nisamehe bure haikuwa nia yangu. Naheshimu sana Imani.
hapana hujanikwaza kabisa kaka....sasa kwa uoni wangu mbona huo utaratibu unaosemea wewe...mifupa ndo inabaki kwa muda mrefu zaidi kuliko kufukia ardhini?!....ardhi inakula mifupa na wala haiwezi kubaki hivyo kwa muda mrefu...lakini hapo naona mifupa ya kutosha na haitoisha leo wala kesho...
 
N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,530
2,000
hapana hujanikwaza kabisa kaka....sasa kwa uoni wangu mbona huo utaratibu unaosemea wewe...mifupa ndo inabaki kwa muda mrefu zaidi kuliko kufukia ardhini?!....ardhi inakula mifupa na wala haiwezi kubaki hivyo kwa muda mrefu...lakini hapo naona mifupa ya kutosha na haitoisha leo wala kesho...
Hvi mifupa huwa inaoza kwa muda gani ardhini nadhani inachukua muda mrefu sana kwa hiyo kama ni hivyo ina maana baada ya miaka labda 1000 tuseme eneo kama Kinondoni makaburini inawezekana kizazi cha wakati huo kikaamua kupatumia kwa matumizi mengine kwa sababu kuna uwezekano ndugu jamaa na marafiki wakawa wameshapoteza historia ya makaburi hayo na uzao umeshatawanyika...kwa hiyo mimi bado nawaza kwamba kama tunataka kuweka historia kwa generations nyingi zijazo labda miaka 100 ijayo makaburi yote ya katikati ya mji yenye umri wa miaka 100 au 90 tuseme yanafukuliwa na mabaki ya mifupa kutunzwa kwa mtindo huu ili pale wazikwe wengine au paendelezwe.
 
tatizo watu wanajengea na siku hizi naona wanazika kama wanavyochimba makaro ya maji....tiles ,zege nzito nondo n.k utaratibu mbaya ulioje...
 
Zesh

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
15,136
2,000
Mkiishiwa maeneo ya kuzikia huko dar mje mzike Lindi huku, eneo kubwa la mkoa wa Lindi ni pori
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
14,972
2,000
Sheikh Ponda anawasikia tu mnaotaka kuzidhalilisha maiti za kiisilamu. Kwani hamkumbuki alivyouwasha moto wakati makaburi ya pale Ilala yalipokuwa yameanza kuhamishwa?
 
Ng'wanamalundi

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
689
1,000
Mwili wa ndugui aliyekufa unakusaidie wewe. Tunahitaji kuchukua tahadhari na ardhi yetu. Tunazika hovyo sana. Kuna kila sababu ya kuchukua hatua ili kunusuru maeneo ya uzalishaji.
Kama huhitaji kujua mwili wa ndugu yako basi ni bora kuchoma moto kabisa ukahifadhi majivu kidogo chumbani kwako. Hiyo ni afadhali kuliko kuweka fuu la kichwa cha nduguyo kwenye kaburi la pamoja kama unavyopendekeza.
 
TsafuRD

JF-Expert Member
Sep 29, 2013
1,958
2,000
huko tunakoenda huo utamaduni wa kuzika hovyo utakoma. Adrhi hii haiongezeki na sisi tunazaliana kwa kasi kubwa sana. Tunahitaji Zaidi ardhi ya kuzalisha na kujenga kuliko ya kuwekea mizoga. Lazima ifike hatua tuzike kwa kubana matumizi ya ardhi. Ukishakufa kinachobaki ni mbolea.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom