X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,399
- 14,313
MAPENZI NI MATAMU, NAOFIA KUUMIZA MOYO
NASHINDWA KUJARIBU, ROHO INANIUMA SANA...
ROHO INANIUMA ENH, ROHO INANIUMAAAA,
ROHO INANIUMA, ROHO INANIUMA,
ROHO INANIUMA ENH..
NAHOFIA KUUMIZA MOYOOOOO, BILA HATA KUPEWA POLE.
DUDU LIUMALO KWANINI NILIPE KIDOLE, OH MOYO
ROHO INANIUMA MIYE.{ KIITIKIO CHA KWENYE WIMBO WA FID-Q_FOHO}
Nimekaa nyumbani nikawa nawaza mahusiano yangu machungu, ya mapenzi niliyowahi kupitia huko nyuma,
najua hakuna ambaye hajawahi kupita kwenye kipindi kIgumu cha maumivu au kidonda kibaya cha mapenzi. kipindi cha maumivu ya mapenzi hufanya mtu awe kama kichaa na mbaya zaidi kichaa wa mapenzi huwa anajijua kabisa kuwa yupo kwenye uwendaazimu, utashindwa kula, kutwa unalia...ukijaribu kulala usingizi hauji...akili inakuwa kama haifanyi kazi...
wengine maumivu ya mapenzi huwapelekea hadi kugombana na ndugu, kuacha kazi zao za maana kisa tu haya mapenzi.
si dhani kama kwa karne za hivi sasa kuna mtu ambaye hajawahi kuumizwa kwenye mahusiano....
nakumbuka
"kulikuwa na kijana anaitwa STUNTER alikuwa na uwezo wa kifedha kutokana na biashara zake za mbao alizokuwa anazifanya, ikatokea siku moja STUNTER alikutana na miss chagga alikuwa ni mrembo, miss chagga alimvutia sana STUNTER ,tatizo moja tu alilokuwa nalo miss chagga alikuwa teja wa madawa ya kulevya na alishawahi kuwahadithia baadhi ya marafiki zake kuwa chanzo cha yeye kukithiri kutumia madawa ya kulevya ni maumivu ya mapenzi. kwakuwa STUNTER alikuwa na uwezo mkubwa tu ki fedha aliamua kumsaidia miss chagga ili baadaye akipona kutoka kwenye uteja wa madawa waoane. kweli jitihada za STUNTER kwa miss chagga zilizaa matunda. miss chagga alipona kabisa urembo wake wa asili alionao ulijidhihirisha kiukweli alivutia sana. STUNTER aliamua kumsomesha miss chagga kwakuwa miss chagga alikuwa na ufaulu mzuli kidato cha sita hawakupata shida ya kutafuta chuo miss chagga alianza chuo kwa msaada mkubwa sana wa STUNTER ....
miss chagga alifanya vizuri kwenye mtihani wake wa mwisho pale chuoni akapata GPA {alama/marks} za juu sana. kipindi hicho kwa ufaulu mkubwa kama alioupata mashirika yalikuwa yanakutafuta yenyewe hivyo miss chagga alipata kazi yenye mshahara mnono alipewa gari na nyumba. kiukweli upendo kwa STUNTER ulizidi walipendana na walihaidiana kuoana hivyo walikuwa wapo kwenye maandalizi ya kuoana.
bahati ilikuwa upande wa miss chagga kwani alichaguliwa kwenda nje ya nchi kuongeza elimu STUNTER hakuwa na jinsi aliamua kumruhusu mpenzi wake aende, miss chagga alipoenda nje alisahau fadhira zote alizofanyiwa na STUNTER. mawasiriano baina ya STUNTER na miss chagga yalikatika kabisa. STUNTER alichanganyikiwa sana msichana aliyempenda, aliyemthamini, aliyemuonyesha kila aina ya starehe, aliyemsaidia leo ameondoka amemuacha peke yake, tena mbaya zaidi amemuacha jangwani bila kumpa ata maji ya kunywa.
STUNTER alilia akakosa wa kumfuta machozi, hakuona ladha ya chakula kwani alishazoe kula pamoja na kipenzi cha moyo wake miss chagga
siku moja STUNTER alipata taarifa kuwa miss chagga anarejea kutoka ughaibuni na nia ya kurejea kwake ni kuja kuolewa...ni kama hiyo taarifa ilikitibua kidonda cha mapenzi kilichokuwa kimeanza kupona cha STUNTER
zile taarifa zilikuwa za kweli miss chagga alirudi bongo akiwa na mshana jr kama mumewe mtarajiwa, STUNTER alifanya jitihada za kumtafuta miss chagga jitihada zake zilifanikiwa.
kumbe kuna kitu kikubwa STUNTER alikipanga, siku aliyokutana na miss chagga , STUNTER aliMfuata miss chagga akamkumbatia kwa nguvu lakini baada ya STUNTER kumuachia miss chagga alianguka kama gunia.. STUNTER alimuua miss chagga ....kipindi hayo yote yanafanyika mshana jr , LEGE , miku pamoja na little hulk walikuwepo eneo la tukio, walimvaa STUNTER wakampiga sana lakini Nifah , Mondray , The Boss na mitale na midimu ambao walikuwa ni maaskari waliwahi eneo la tukio wakamkamata STUNTER
wivu wa mapenzi ulimfanya STUNTER asote gerezani miaka 7 hakuomba kutoka, hakujutia kufanya hicho alicho kifanya lakini alijutia wema wake aliomfanyia miss chagga.
siku ya hukumu ilipofika mbele ya hakimu Daby , STUNTER alikuwa anashitakiwa na jamhuri kwa kosa la mauaji.. nameless girl na Shunie ambao walikuwa ni mawakili walijitolea kumtetea STUNTER
hakimu Daby alilizishwa na hoja za wakili Shunie kuwa mtuhumiwa kipindi anafanya mauaji hakuwa na akili timamu na kutokana na polisi kutokujua majukumu yao hawakumpeleka STUNTER kupimwa akili....wakili nameless girl nae akaesema kuwa jamhuri itoe visibitisho ambavyo ni kisu na zile nguo zenye damu zitakazoonyesha kuwa ni kweli mtuhumiwa alifanya kosa....hoja hizo zenye msingi zilimfanya STUNTER aachiwe huru...
alikuwa huru lakini hakuwa na kitu, hakuwa na mali wala pesa, ndugu jamaa na marafiki zake wote walimgeuka na kumuona muuaji. STUNTER alichanganyikiwa..... na mbaya zaidi alikuwa CHIZI TENA CHIZI WA MAPENZI"
najua nawewe msomaji uliwahi kuumizwa kwa namna moja ama nyingine....najua unayo mengi ya kutuhadithia...naomba utuambie kuwa ilikuwaje hadi ukajikuta una kidonda kikubwa cha mapenzi, ni kitu gani hutokisahau tokea ulivyoumizwa kwenye mapenzi...je unajutia au umeona ni bora ulivyoumizwa kwani umejifunza kutokana na kuumizwa?
lengo ni kutoa funzo kwa wengine wanaojiingiza kwenye mahusiano
{ N.B STORY HII HAIHUSIANI NA MAISHA HALISI YA MARAFIKI AMBAO MAJINA YAO NIMEYATUMIA KWENYE HADITHI HII }