Ili kundi lisiache kuombewa pia

pureman2

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
1,494
2,538
Najaribu kuwaza kwa sauti

Maishani, kila mmoja amebeba kusudi la kuishi kwake. Wakati mwingine mhusika anaweza asijitambue vyema ila watu wengine wakatambua umuhimu wa mtu huyo katika maisha ya kila siku.

Leo nataka nitafakari na wewe kuhusu mchango wa wataalamu wa afya, medical scientists, namna mchango wao unavyofanya dunia hii kuwa mahala sahihi pa kuishi.

Tafakari kusingekuwa na ugunduzi wa chanjo mbalimbali zinazotolewa kudhibiti magonjwa mbalimbali na hata vifo vya haraka. Chanjo ya polio, homa ya mapafu, pepopunda, dondakoo, surua, kifua kikuu, homa ya ini etc. Kusingekuwa na chanjo kama hizi inakadiriwa robo tatu ya watoto wangekuwa wanakufa kabla ya kusherekea birthday yao ya tano ya maisha (under 5 mortality).

Tafakari kusingekuwa na uvumbuzi wa madawa kama antibiotics, antifungal and anti helminthic, zinazotumiwa duniani kote kutibu infectious diseases, magonjwa ya kuambukiza yatokanayo na vimelea vya bacteria, fungus,na minyoo. Kusingekuwa na ufumbuzi wa madawa haya muhimu inakisiwa zaidi ya robo tatu ya dunia ingekuwa kwenye maradhi makali na pengine survivor ingekuwa sehemu kidogo sana kwa population ya dunia.

Tafakari kama kusingekuwa na uvumbuzi wa madawa ya ARV na TB, zaidi ya theluthi ya population ya nchi zilizo chini ya jangwa la Sahara ingekuwa imesharudi kaburini. Najaribu kuwaza maumivu na umasikini wetu jinsi ambavyo ungekuwa umelifunika bara hii.

Najaribu kuwaza kusingekuwa na doctors, nurses, lab scientists, wafamasia na wataalamu wa afya wengine, ambao wanafanya kazi usiku na mchana kuokoa majeruhi wa majanga mbalimbali kama ajali za magari, majanga ya asili, majaribio ya kujiua kwa sumu na vitu vingine. Piga picha watoto kwa wakubwa wenye mauvimbe na matatizo yanayohitaji upasuaji kama kusingekuwa na interventions za wataalamu wa afya sijui maisha ya dunia hii yangekuaje?

Piga picha wa mama wajawazito wenye changamoto ya uzazi pingamizi alafu kusiwepo msaada wa daktari na mkunga?

Nisikuchoshe sana kwa leo, kuna picha nadhani umeipata.

Asante Mungu kwa kuumba watafiti, wanasayansi, best brain waliofanya na wanaoendelea kufanya ugunduzi ulioleta majibu kwa changamoto lukuki za kiafya duniani.(kwa sehemu kubwa wazungu -Mungu awabariki sana).

Asante Mungu kwa kubariki watu binafsi, serikali, viwanda, makampuni makubwa ya dunia na kanda, jumuiya za watu wenye mapenzi mema ambao kwa moyo wao wa kupenda ujitolea kuchangia fedha zao ili kuhakikisha tafiti na huduma za tiba na afya zinapatikana duniani, na kuhakikisha huduma za afya zinatolewa.

Kundi la watu wanaoshiriki kazi hii ya kiuumbaji na kuboresha afya za watu duniani kote, ndilo kundi kwenye maisha yangu yote nimelichagua kuliombea kila nipatapo fursa ya kupiga magoti kumuomba Mungu.

Kazi yenu ni njema sana kwa ustawi wa jamii. Msizimie moyo hata kama kuna changamoto lukuki mnazipitia.

Toa mtazamo wako tujifunze sote.

Kind regards.
 
Pata picha pia kusingekuwa na mafundi ujenzi!
Angalia jinsi muonekano wa mazingira na maisha yote vile yangeonekana.
Umeona?
 
Tukizidi kushukuru itabidi hadi Jua mvua na makitu kibao tuyasifie maana bila jua hata uhai hapa dunian usingekuwepo.
 
Tukizidi kushukuru itabidi hadi Jua mvua na makitu kibao tuyasifie maana bila jua hata uhai hapa dunian usingekuwepo.
Daah ...Mungu fundi

Ukiwa unatafakari hivi maisha haya u must be grateful
 
Back
Top Bottom