MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,221
- 22,292
ILI KUEPUSHA MAJANGA KWENYE NDOA TURUDI KWENYE MILA ZETU
Siku hizi watu hawazingatii kabisa mambo ya kimila. Tumewadharau sana wazee wetu ndo maana majanga kila siku kwenye ndoa.
Enzi zetu ukitaka kuoa kuna njia mbili; aidha uchague mchumba wewe mwenyewe au wazee wakuchagulie.
Na kabla ya ndoa lazima tambiko lifanyike ili mizimu itoe kibali. Tambiko huwa ni la siku tatu ambapo wakati wote wa tambiko chakula kikuu ni supu ya mkia wa kondoo ambayo haijawekwa chumvi.
Pia kwa siku hizo tatu hakuna kuoga wala kuvaa viatu. Na ikitokea wazee wamekuchagulia mchumba basi hutamwona huyo binti hadi siku ya ndoa tena jioni maana muda wote kafunikwa usoni.
Na kama una bahati unaweza kukuta tayari ana mimba kwahiyo mtoto anahesabiwa ni wa kwako.
Nadhani ili kuepusha majanga turudi kwenye mila zetu.