Ile Kadhia ya Mzee wa Vijisenti iliishia wapi

Ile Kadhia ya Mzee wa Vijisenti iliishia wapi

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,760
Kamati ya Uandishi inajumuisha wajumbe 24 wakiwamo watu wazito na inaongozwa na Mwanasheria Mkuu mstaafu, Andrew Chenge na mjumbe mwingine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema na wanasheria mbalimbali waliobobea katika taaluma ya sheria.

Nimeshangaa sana kuona huyu mtuhumiwa ambae aliweka dharau ya ainayake kuhusiana na mihela aliyoificha huko majuu ,naona mbali ya kuwa na dharau amepewa uongozi wa kamati ,Je mtu huyu hakurubuniwa kupitisha au kuhakikisha mikakati ya CCM inapita bila ya kupingwa ,kama akisitasita na kubabaika atashughulikiwa kikamilifu kutaifishwa na kutupwa jela ?

Sasa ikiwa huyu ni mmoja mwenye kesi dhidi ya uhujumu uchumi ,je tujiulize wamo wangapi wa aina yake wamechomekwa kulihujumu Taifa katika kupata KATIBA safi ,hivi mtakosa majangili ? Mtakosa wakwepa kodi ? Wote wa dizaini hii ikiwa wamo wamejalizwa ili kuhakikisha matakwa ya CCM yanapita ,mbali ya wabunge na wawakilishi wa CCM ambao walishinda ubunge na uwakilishi kwa msaada wa tume za uchaguzi za CCM ,hivi watu wa kusaidiwa namna hii watawezaje kutetea wananchi ikiwa wamepewa maagizo ya kufanya juu ya mikakati ya maslahi binafsi ya Chama Chao ,ikiwa kutasemwa watu hawa wametishwa na kupewa onyo kama watakengeuka Chama kitawashughulikia na kuwapiga na chini na hata kuwawekea mizengwe katika shuguli zao ,tumeona yaliyomkuta Mansour Yousuf ameenda kinyume na Chama ameshughulikiwa ,sasa watu hawa wa CCM waliojazwa ndani ya Bunge watu ambao kuwepo kwao kwenye nafasi za ubunge na uwakilishi ni wa kutiliwa mashaka ,watawezaje kulipatia Taifa Katiba ,ndio maana CCM kwa kuona ina watu wake ambao imewamiliki itawatumia kuupitisha Katiba wanayoitaka iwalinde.

Lao hii kila mtu anaona ni jinsi gani bunge limevurugika sababu kuu ni kuwemo kwa watu waliopata vyeo kwa kufadhiliwa na kushinda kwa kutumia mgongo wa tume ya Uchaguzi ya CCM na si kwa ridhaa za wananchi waliopiga kura.

Inakuwaje kuwaje leo akina Chenge ,akina hamad rashi watu wenye matatizo na vyama vyao kupewa ukuu ,tunamuona Hamadi Rashidi anavyojitutumua kulinda maslahi ya CCM hana hata aibu anajua akikosea tu vitega uchumi vyake vitasambaratishwa ,hii ni aibu kubwa kwa Mkuu wa Nchi kushindwa kuyaona haya as the President wa nchi na sio Chama.
 
huyu atakwenda the hague na wenzake wote walioifilisi nchi hii.
 
Back
Top Bottom