"Ikumbayaga Gold Rush" kisima kipya cha dhahabu chagunduliwa mkoani Geita.

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
11,641
2,000


Kumegunduliwa dhahabu katika mtaa wa Nyanza katika kijiji cha Ikumbayaga kilichopo kilomita 3 kutoka mjini Geita.

Mtaa huo wenye watu wapatao 1000 ghafla umekuwa na shamrashamra khasa baada ya sherehe za uhuru wa Tanzania na katika kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru wananchi wa mtaa wa Nyanza wameamua kutoondoka kwenye neo hilo.

Eneo ilipogundukila dhahabu hiyo lipo ndani ya shamba la mwanakijiji mmoja aitwae Juma Kyoma ambae alihamia mahali hapo mwaka 1996. Kwa miaka 20 alokaa hapo bwana Kyoma hakuwahi kuona mwekezaji yoyote yule akifanya shughuli zozote za uchimbaji katika eneo hilo.

Bwana Kyoma akishirikiana na wananchi wenzake wapo katika hatua za mwisho za kuunda umoja wao wa Saccos ya Ikumbayaga ili kuweza kupewa leseni halali na kuanza kazi rasmi ya kuchimba madini hayo katika eneo hilo.

Hata hivyo, ofisi ya madini ya mkoa imeonekana kutotoa ushirikiano wa kuridhisha juu ya kushughulikia maombi ya leseni lakini ofisa madini mkazi wa wa mkoa wa Geita bwana Fabian Mshai amekiri kugunduliwa kwa madini ya dhahabu katika eneo hilo na kwamba idadi ya watu 3000 watanufaika na madini hayo.


Maisha halisi ya Ikumbayaga kwa sasa.

Nao mkuu wa Mkoa wa Geita meja jenerali mstaafu Elias Kyunga na mkuu wa Wilaya ya Geita bwana Herman Kafupi wamekiri kuwepo kwa ugunduzi huo na wametoa ahadi ya kuwasaidia wananchi hao kupata leseni ya uchimbaji madini hayo na pia kuwahakikishia kuwa hawatahamishwa katika eneo hilo ili kupewa wawekezaji wa nje.

Huu ni wakati sasa wa wananchi wengine na wajasirimali wa Tanzania kuitikia wito huu wa "Ikumbayaga Gold Rush" kwa kuelekeza nguvu zao kijijini Ikumbayaga ili kuanza kufanya shughuli za maendeleo katika eneo hilo na hatimae kusambaza maendeleo katika mkoa mzima wa Geita.

Wananchi hao wa Ikumbayaga wanaweza kuwa wamegundua dhahabu katika eneo hilo lakini wakawa wanakisa vifaa muhimu vya kuwezesha uchimbaji wa kisasa, na hata kama vifaa hivyo na utaalam vitakuwepo kwa kiwango cha kati, bado kuna matumaini makubwa kwa wananchi wa Ikumbayaga na wengine wa mkoa wa Geita.

Fedha itakayotokana na dhahabu ya Ikumbayaga inawezesha kujengwa kwa miundo mbinu mingi ikiwemo barabara za kisasa, madaraja, shule, hospitali, majengo ya hoteli na migahawa, kumbi za starehe na shughuli zingine lukuki za kibiashara.

Serikali kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ya Geita wana budi kusimamia kwa dhati ugunduzi huu wa dhahabu ya Ikumbayaga na kuhakikisha kwamba kila mwananchi wa Ikumbayaga ananufaika kwanza kabla ya maendeleo katika meneo mengine kushika kasi.

Tuunge mkono "Ikumbayaga Gold Rush" au makimbilio ya dhahabu ya Ikumbayaga.

Mungu ibariki Ikumbayaga, Mungu ibariki Tanzania.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom