Kweli Ikulu yenu haina kazi! Si wangenyamaza tu maana hii ni aibu kwao. Hebu nisaidieni, hivi huyu Salva ni yule mwandishi wa habari ambaye mkewe aliandikwa kwenye Daily News kuwa alijilipua (alichana passport ya Tanzania) Uingereza na kudai ati ni mkimbizi wa kisiasa? Je, nini status ya mkewe siku hizi? Bado ni mkimbizi? Ama kweli JK kiboko, hivi kama vetting ingefanyika kweli unaweza kumteua Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu ya nchi mtu ambaye mkewe kaikimbia nchi hiyohiyo tena katika mazingira tata? Ni Bongo pekee ambapo mtu na mdogo wake wanateuliwa Waziri na Katibu Mkuu (ama Naibu Waziri) wizara moja. Kweli usalama wa taifa umekuwa usalama wa Nyinyiemu