"IKO WAPI ZAMANI??"

Arabian Eagle

Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
71
Reaction score
46
Habari wana Jf.

Leo nimekumbuka na mengine kuhadithiwa ya zamani na nimejikuta nimeipenda zamani kuliko zama za sasa.

Zamani ilikuwa mkikutana mahala basi naam mtaongea stori nyingi na kufurahi, lakini leo hii mkikusanyika zaidi ya watu wawili hakuna stori wala kila mmoja kainamisha kichwa chini yeye na simu tu.[emoji848]

Zamani ilikuwa watoto wanacheza michezo ya kombolela, ukuti, kupeana vitendawili vya shule, mafumbo, kusimuliana hadithi N.k lakini leo hii watoto wa zama hizi hawafanyi vitu hivyo
[emoji848]

Zamani vijijini, majirani walikuwa kama ndugu walikuwa wakipeana vyakula na hata kula pamoja.. lakini sasa hivi ni yarrab nafsi.

Zamani kwa waislamu kipindi cha mwezi mtukufu kwa sisi tuliokulia vijijini ilikuwa muda wa kufturu futari inaliwa nje si ndani kama wafanyavyo sasa.

YAPO MENGI YA ZAMANI YANAYOFURAHISHA KULIKO YA SASA.
WAWEZA ONGEZA MENGINE IKIPENDA.

@arabian_eagle.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…