Iko haja kwa ratiba za masomo elimu ya msingi ziishie saa nane kamili

Jun 29, 2013
64
19
Baada ya usitishwaji wa michango elekezi kwa wazazi wa watoto shule na msingi na sekondari, kumekuwa na lalamiko kuu la kwa shule nyingi zinashindwa kujimudu hasa katika kuwaandalia watoto chakula cha mchana mashuleni.

Kwa mtazamo wangu sioni haja ya kuwepo kwa mchango huo wa chakula kwani kuna sababu yeyote ya msingi watoto hapo kushindwa kuhudumiwa na wazazi wao moja kwa moja kama ilivyokuwa hapo awali.

Pia iko haja ya ratiba za masomo kurudi kama ilivyokuwa hapo awali kuwa masomo yanaanza kuanzia SAA mbili na kutoka SAA nane. Hapo ni kwamba watakuwa na breaks mbili SAA nne watspumzika dakika 15 na SAA sita watapumzika dakika 30.

Sisi tulisoma kwa mfumo huu na wala hatukuwa tunahitaji chakula kitoke shuleni. Watoto kuwapa chakula cha mchana mashuleni ni uzembe na uwoga mkubwa usio na sababu ya msingi.

Kwani tumeendelea kuna licha ya kuweka mfumo kuu wa kuwapa watoto cha kuna shuleni hakuna mabadiliko yeyote kitaaluma bali ni kushuhudia kushuka kwa elimu nchi mzima.

Naona iko haja ya kuurudia mfumo wa awali utasaidia kuondoa mapungufu yaliyopo na kuwafanya watoto kuwa makini kitaaluma. Mi yangu ni hayo tu katika kuinusuru elimu ya Tanzania.
 
Halafu wazazi wengi hawajui tu baada ya chakula cha mchana hakuna somo linalopanda zaidi ya wanafunzi kulala lala tena usiombee ukute baada ya msosi ni hesabu class yote watu wanakuwa wamelala...nakuunga mkono bora wanafunzi wamalize masomo saa nane tu
 
Back
Top Bottom