hippocratessocrates
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 3,598
- 1,540
Kumbe ndio maana unaitwa 'chilisosi' - maanake unawasha lakini wenzako bado wanakula!!! Umeshindwa kuelewa ya kwa kwamba CCM ina list ndefu kama bara bara ya kukimbiwa na viongozi wake? nitakusaidia kukumbusha:
1. Edward lowasa - alikuwa Waziri mkuu TZ na mjumbe wa CC na NEC ya CCM
2. Fredrick Sumaye- alikuwa waziri mkuu TZ namjumbe wa CC na NEC ya CCM
3. Mgana Msindai- alikuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM wa mikoa
4.Seif Sharif Hamad - Alikuwa Waziri kiongozi wa SMZ na mjumbe wa CC na NEC ya CCM
5. Hamad Rashid Mohd- alikuwa waziri wa TZ na mjumbe wa NEC ya CCm
6. Mansour Yussuf himid- alikuwa waziri wa SMZ na mjumbe wa halmashauri ya CCM
7. Khamis Mgeja alikuwa mwenyekiti wa CCM wa mkoa Mwanza
7. Makongoro Mahanga _waziri wa serikali ya CCM
8.lawrence Masha - waziri wa serikali ya CCM
9.James Lembeli - Mbunge wa CCM
10. Ester Bulaya - Mbunge wa CCM
11. Mzee Hassan Moyo- Mwanachama muanzilishi wa CCM mwenye kadi namba 7!!!
Hao niliokutajia basi ni viongozi wachache tu ambao wameondoka CCM hivi unataka kutueleza ya kwamba wewe unauchungu na CCM kuliko hao? najua uko CCM kwa maslahi yako lakini kumbuka unapomwonyesha Kidole mwenzako basi ujue ya kwamba vidole Vinne vinakuangalia wewe. Toka huko CCM unangoja nini??? Au huko kwenye CCM ndio kuna wale walaji wa Chilisosi?
Very useful post. Halafu huyu bwana mdogo hajui hata Wassira alikuwa chama gani! So pathetic.