Wana JF,
Kwanza niseme mimi ni Mkristu na Ijumaa Kuu inamaana kubwa sana kwetu wakristu.
Kwa sababu ni siku muhimu sana kwa wakristu lakini pia ni siku muhimu kwa waislamu wote maana ndio siku ya ibada kwao.
Kwa kipindi cha miaka 17 kuna watanzania wengi wamepata madhila mbali mbali, wameuwawa kwa namna mbali mbali na wauwaji wameshindikana kupatikana.
Kwa kipindi hicho kuna watu walitekwa na kuteswa kwa namna mbalimbali bila watesi hao kupatikana, kuna watu wamekamatwa na kufungwa pasipokuwa na kosa na wengine kusingiziwa makosa ambayo hawakuyatenda wao.
Kuna watu walipata vipigo na mateso makali na polisi pasipokustahili mateso hayo. Hawa wote walipitia mateso hayo sio tu ymewaumiza wateswa bali familia zao, ndugu na jamaa zao, wanajamii kwa ujumla.
Lakini pia wale waliokufa wanahitaji kupata huruma ya Mungu, Mungu awapokee kwenye ufalme wake kupitia sala zetu ili yale machache waliomkosea maulana wangali hai waweze kusamehewa.
Kundi ama makundi yaliyokuwa yanafanya utesaji, uuaji na kusingizia bado yapo kwenye jamii zetu leo wamefanyiwa jamaa zetu kesho ni yeyote miongoni mwetu
Hivyo ni jukumu letu sote kwa imani yoyote uliyo nayo siku ya ijumaa tufanye sala maalum.
Kwanza tuwaombee wale wote waliopoteza maisha yao Mungu azipokee roho zao.
Pili wale wote walioteswa, kusingiziwa na kuumizwa kwa namna moja amazingine apate moyo wa kusamehe kama Kristu alivyomsamehe Yuda aliyemsaliti Yesu na ndio maana tunaadhimisha sikukuu ya pasaka kwani ndio kiini cha Ukristu wetu na iman zetu.
Tatu tuwaombee kwa mwenyezi Mungu wale wote waliotenda hayo wafanye toba na kumrudia Mungu na kukiri makosa yao na wabadili mienendo yao.
Kubwa zaidi tuwaombee wale ambao bado mioyo yao migumu Mungu awape adhabu kali kwa kadiri anavyoona inafaa. Hapa ni muhimu maana ndio njia pekee ya sisi kuendelea kubaki salama
Ombi kwa madhehebu yote ya kikristu na kwa ndugu zetu waislam, wahindu na wengine tuombe kwa pamoja hiyo ijumaa, kila mmoja afunge na kuomba ili yasimpate hata mmoja wa wanafamilia yake yale yaliyowapate wenzetu, pili tuziombee familia zingine nazo zisipate mateso tena. Na kubwa tuwaombee watesaji Mungu awabadili mioyo yao na hata kuwapa adhabu kulingana na stahiki zao.
Sisi kwa umoja wetu tukiomba japo Dakika tano kwenye sala za jumuiya naamini tunaweza kubadilisha mtazamo wa watesaji.
Tukumbuke Mungu hajawahi kushindwa lakini pale tunapomlilia kwa imani na kweli basi hutenda kwa kadiri anaona inafaa.
Ijumaa kuu tupaze sauti zetu kwa Mungu ili watesi wetu waumbuke