Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 32,062
- 43,488
project ara ni kazi mpya ya google ambayo lengo lake ni kutengeneza simu ambayo itakua inaundwa na vipande vipande vya hardware mpaka inakamilika. project hii ilianzishwa na motorola lakini google walivyoiuza kwa lenovo hii project ikabakishwa. project hii pia itakuwezesha wewe mtumiaji kuweza kuunda simu unayoitaka sababu simu inakua haina umbo moja bali ni vipande vipande.
ninaposema vipande vipande namaanisha nini?
hii itakuwa ni open source ya hardware inamaana kila kampuni itatengeneza vipande vyake halafu vinaunganishwa kutengeneza simu. kutakua na vipande kama,
1. kipande cha battery
2. kipande cha kioo (display)
3. kipande chenye ram na processor
4. kipande cha spika na mic
5...............................
kuna mambo 10 unatakiwa uyajue ili kuielewa na kuipenda hii project.
jambo la kwanza ni bei
simu hii itaanza kwa bei rahisi tu ya dola 50 (elfu themanini) lakini utaiupgrade mwenyewe kwa kuongeza vipande vyako. mfano ina storage 4gb na ram 512mb basi utaweza kuchomoa kipande cha memory, ukanunua chengine chenye storage 16gb na ram 2gb. pia kutakuwa na simu ya dola 500 kwa wale wanaopenda mambo ya luxury.
jambo la pili ni upatikanaji
simu hii itaanza kupatikana mwanzoni mwa mwaka 2015 hivyo itabidi usubiri kidogo.
jambo la tatu ni ukubwa
simu hii itakua na ukubwa wa kawaida kama wa s5 hivi yani inch 5 lakini kutakuwa na mini yake kwa wanaopenda visimu vidogo na kutakuwa na kubwa zake kwa wale wanaopenda minyambizi kama galaxy note.
jambo la nne ni module
hapa inabidi uwe makini kuielewa vizuri hii project nitaelezea kiurahisi kidogo unatakiwa ujue vitu vitatu
1. module- hii ndio vipande vipande
2. endo - hii ndio chasis aka eneo vipande vinapoungiwa
3. sumaku - kigandisho
hebu tuangalie hii picha
jamaa kwenye picha ameshika simu na kioo cha simu amekitoa. hio chasis ya rangi ya kijivu/nyeupe ndio endo na hiko kioo ndio module hivyo kioo kinaganda kwenye endo kupitia sumaku. kwa mfumo huo huo unaweza gandisha vitu vingi.
jambo la tano ni ununuzi wa module
tumeona module ni vipande vipande vinavyonatishwa kwenye simu yetu hivyo tutakuwa tunavinunua. google wataanzisha market kama playstore utaweza kununua online. mfano labda sharp atatengeneza module yake ya kioo halafu atapost playstore samsung nae atatengneza module ya memory nae atapost.
jambo la sita ni operating system
sababu ni google os itakuwa android, lakini android ya sasa haikubali simu za namna hii hivyo google wamesema ikifika 2015 watakuwa wamesha update android kutumika kwenye hizi simu.
jambo la saba ni prototype
google walishindwa kutuonesha mfano wa simu inayofanya kazi, ila wapromise mwezi wa 9 tutaiona hio simu. mwez huu wa nne walionesha mfano wa simu ila bila sumaku na kioo kilikuwa kimepasuka.
jambo la nane ni module zitakuwa na matumizi mengi
ok watanzania hatuwezi kutengeneza simu basi hata module tushindwe? hapa watanzania tunaweza tengeneza module yenye tochi, futi ya kupimia na hata rimoti za tv ili kufanya simu zikae kibongo bongo.
jambo la tisa kwanini ujali?
google wamesema simu hizi zitadumu miaka 5 hadi 6 hivyo kuwa simu nzuri na zisizopitwa na wakati.
jambo la kumi kwa nini madeveloper wajali?
madeveloper watapunguza cost za kudesign hardware zao maana kazi itafanywa na google wao wataeka tu innovation zao.
hii ndio project ara je umeipenda?
source
mimi na http://thenextweb.com/google/2014/04/15/googles-project-aria-modular-smartphones-get-rollout-date