PreGE2025 Ijue nguvu ya kelele Katika kuangusha ngome ya adui wa wananchi kuelekea uchaguzi mkuu 2025

PreGE2025 Ijue nguvu ya kelele Katika kuangusha ngome ya adui wa wananchi kuelekea uchaguzi mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,938
Reaction score
41,098
Hellow!

Utapingana na Mimi kama hujawahi simama Katika umma wa wananchi kama kiongozi, ila utakubaliana nami kuwa Katika halaiki yoyote, kelele za umati wa watu kushangilia au kuzomea zina nguvu kubwa sana Katika kuongeza ujasiri au kuingiza hofu kwa kiongozi asimamaye jukwaani.

Niliwahi kushuhudia umma wa wananchi ukimpigia kelele hayati Nyerere alipokuwa jukwaani akimnadi Hayati Mkapa jukwaani, Kila alipojaribu kuongea kelele ziliongezeka, Kila alipoinua kifimbo chake kutuliza sauti zile ,sauti hazikukoma, ilifika time wapiga kelele wale walienda kumchukua mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Kiboko Nyerere Ili aje kuongeza kelele Katika mkutano ule, baada ya kelele kuzidi alipofika ndugu yule, Mwalimu alisikika akisema nilidhani Niko Kenya, na baada ya kusema hayo, aliteremka jukwaani na mkutano uliishia pale. HAYO yalitokea mwaka 1995 kwenye kuanza mfumo mpya wa vyama vingi, Mrema akiwa mgombea wa upinzani uwanja wa Mukendo Primary School.

Mji wa Yeriko uliangushwa kwa kelele za sifa kwa Mungu mkuu, kelele ziliingiza hofu kwa maadui wakakosa Cha kufanya. Hilo linarufunza nguvu ya kupaza sauti kuzomea au kushangilia.

(Zaburi 137:4)
Tutaimbaje wimbo wa BWANA Katika nchi ya ugeni( utumwani),
Nchi inahujumiwa na kufilisiwa, tutaimbaje wimbo wa furaha Katika nchi yetu?

Kuelekea Katika majukwaa mbalimbali ya kisiasa 2025, wananchi wanatakiwa kupiga tu kelele, kelele ni kelele,

Kuimba ni kelele,

Kulia ni kelele pia,

Kuzomea ni kelele pia,

Kushangilia ni kelele pia.

-Martin Luther alipiga kelele Amerika ikasikia,

-Desmond Tutu alipiga kelele, ubaguzi wa rangi ukayeyuka,

-Mwl Nyerere alipiga kelele ya haki, nchi ikazukiwa na Nuru, tukapata uhuru.

-Tundu Antipas Lissu anapiga kelele kutafuta kuondoa haramu ndani ya sanduku la kura. "NO REFORMS, NO ELECTION". Amesikika🔥💪

- Joseph at Gwajima anapiga kelele kudai maono ya nchi yaandikwe ubaoni Ili Kila Rais ajaye asome na kutekeleza maono hayo, SI kila mmoja kuja na lake.

-Rabbon anapambana kuuleta ufalme wa Mungu Katika siasa za nchi yetu, viongozi walevi wa namna mbalimbali wasipate fursa kuongoza watu, haki itawale ,hofu ya Mungu itawale, UOVU utokomee, elimu ishamiri nchi istawi.

Kila asimamaye jukwaani apate kelele anayostahili kulingana na matendo yake.

1. Anayestahili kelele za shangwe, apewe shangwe,

2. Anayestahili kelele za kuzomewa, apewe haki yake.

Karibuni tupige kelele 🙏,
Na hakika adui atakuwa mdogo sana, nguvu zitamwisha, vifundo vya miguu vitakosa nguvu, hatoendelea kutoa hadaa na uongo kwa wananchi Tena.

NOTE: Mtu yeyote asikudangaanye kuwa kelele KUPITIA keyboard JF na majukwaa mengine hazisikiki, kelele ni kelele. Piga kelele.

NRNE 💪 🔥

Nawasiiisha 🙏
 
Asante.
Kuna wengine humu wanasema kisa hatujitokezi kuandamanq kamq KENYA basi tusipige kelele kuunga mkono "NO REFORM NO ELECTION" Wapuuzi hawa wanasema kufanya hivyo ni kumng'ong'a lisu!? Ujinga kabisa kwani lisu anapiga kura peke yake Tanzania?
No reforms no election
 
Niliwahi kushuhudia umma wa wananchi ukimpigia kelele hayati Nyerere alipokuwa jukwaani akimnadi Hayati Mkapa jukwaani, Kila alipojaribu kuongea kelele ziliongezeka, Kila alipoinua kifimbo chake kutuliza sauti zile ,sauti hazikukoma, ilifika time wapiga kelele wale walienda kumchukua mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Kiboko Nyerere Ili aje kuongeza kelele Katika mkutano ule, baada ya kelele kuzidi alipofika ndugu yule, Mwalimu alisikika akisema nilidhani Niko Kenya, na baada ya kusema hayo, aliteremka jukwaani na mkutano uliishia pale. HAYO yalitokea mwaka 2000, uwanja wa Mukendo Primary School.
Nyerere alimnadi Mkapa mwaka 1995 sio 2000.
 
Hellow!

Utapingana na Mimi kama hujawahi simama Katika umma wa wananchi kama kiongozi, ila utakubaliana nami kuwa Katika halaiki yoyote
Kwanza mwaka 2000 Mwalimu JK Nyerere hakuwepo. Alifariki October 14, 1999.
Alafu tukio kama hilo lilifanyikia uwanja wa Obwere, Shirati Rorya mwaka 1995 kwenye kampeni akimnadi BW Mkapa.
Hali ya kelele ilikuwa mbaya hadi akalazimika kumnadi Mabere Marando mgombea wa upinzani!
 
Asante.
Kuna wengine humu wanasema kisa hatujitokezi kuandamanq kamq KENYA basi tusipige kelele kuunga mkono "NO REFORM NO ELECTION" Wapuuzi hawa wanasema kufanya hivyo ni kumng'ong'a lisu!? Ujinga kabisa kwani lisu anapiga kura peke yake Tanzania?
No reforms no election
Hata kelele za kwenye keyboard JF zinasikika,

1. Kelele tulizopiga awali kuhusu " BILA TUME HURU YA UCHAGUZI NA KATIBA MPYA, UCHAGUZI UTAYEYUKA" zimezaa matuda, na CDM inatumia slogan ya " No reforms, no Election.

2. Kelele tulizopiga kuhusu Kurudishwa CHADEMA Dr Slaa, zimezaa matunda.

Tuzidi kupiga kelele, zinasikika.
 
Kwanza mwaka 2000 Mwalimu JK Nyerere hakuwepo. Alifariki October 14, 1999.
Alafu tukio kama hilo lilifanyikia uwanja wa Obwere, Shirati Rorya mwaka 1995 kwenye kampeni akimnadi BW Mkapa.
Hali ya kelele ilikuwa mbaya hadi akalazimika kumnadi Mabere Marando mgombea wa upinzani!
Asante, nimerekebisha.

Upinzani wa 1995 hajawahi tokea,

Labda October 2025 na kuendelea utauzidi wa 1995.
 
Hata kelele za kwenye keyboard JF zinasikika,

1. Kelele tulizopiga awali kuhusu " BILA TUME HURU YA UCHAGUZI NA KATIBA MPYA, UCHAGUZI UTAYEYUKA" zimezaa matuda, na CDM inatumia slogan ya " No reforms, no Election.

2. Kelele tulizopiga kuhusu Kurudishwa CHADEMA Dr Slaa, zimezaa matuda.

Tuzidi kupiga kelele, zinasikika.
Kelele ni kelele haijalishi unazipigia wapi!
Na Bora kelele zipigwe kuliko ukimya!
 
Kelele ni kelele haijalishi unazipigia wapi!
Na Bora kelele zipigwe kuliko ukimya!
Kelele ni kelele,

Kuna watu hupigia kelele chooni kulaumu au kulaani watu wanaowaogopa kuwambia live!

Cha kushangaza, kelele hizo pia husikika! Maana huja kwa mlengwa KUPITIA ndoto.
 
Unamaanisha upinzani wa Lyatonga Mrema (Rip) ndio bora kwako na haujawahi kutokea ?
Ndio, ulikuwa Bora Katika angle zifuatazo,
1. Mwitikio wa wananchi kwenye viwanja vya siasa.

2. Uhuru wa kuongeza bila woga kwa wapinzani.

3. Commitment ya kutaka.mabadiliko ilikuwa juu sana, Mrema gari yake ilisukumwa nchi nzima na wananchi kama ishara ya kutaka mabadiliko.

4. Watu walitoa Mali zao bila kusita kusuppot mabadiliko.

5. Ushamba wa kutekana kuogopa hoja kinzani ulikuwa nadra sana.

Ulikuwepo 1995?
 
Unaamini Mrema Lyatonga (Rip) alikuwa mpinzani wa kweli?
 
Unaamini Mrema Lyatonga (Rip) alikuwa mpinzani wa kweli?
Najua kilikuwa kinyago kilichochongwa na watawala,

Lakini umati, hamasa waliyoonyesha kwake akiwa mpinzani pekee mwenye nguvu, ilitosha kupeleka ujumbe,

Na utaona Aliyofanya Mkapa yalikuwa influenced sana na uwepo wa upinzani kipindi like.

Kelele ni kelele.

Mtoto mdogo akiita mwiziiiii, hata kama mwizi ni mwili jumba, kelele Ile hupunguza nguvu na ujasiri wa mwizi akatimua mbio,

Saaa hawa wezi wa kura waitwe wezi kwa haki na matendo yao live jukwaani, wa kuzomewa wazomewe.

Piga kelele za haki, nchi na mbingu zisikie.

Karibu 🙏
 
Naunga mkono HOJA..CDM endeleeni kuyahusisha makundi mbalimbali ya kijamii, hasa TEC na BAKWATA
 
Naunga mkono HOJA..CDM endeleeni kuyahusisha makundi mbalimbali ya kijamii, hasa TEC na BAKWATA
Uko sawa, japo Mimi sio mwana CDM,

Naipigia kelele CHADEMA Ili nayo ipige kelele zaidi, kelele za haki mbingu na nchi visikie,
Ili hatimaye sanduku la kura liheshimiwe,

Tusijeongozwa na muuza bangi / drugs kwa kuiba kura.
 
Ni kelele zilimfanya hayati Magufuli kukunja ngumi na kupiga push up Ili kuushawishi umma kumpigia kura kwamba Yuko fit kiafya.

Kelele zizidi, chama chakavu kishushe mapanga na kuvua mask Ili ndugu zetu waliopotea warudi kwa baba, mama, na famillia zao.
 
Back
Top Bottom