Ijue maana ya 'wife material'

BRN

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2013
Posts
5,392
Reaction score
6,906
Wakuu habari,

Kuna mazoea tumejijengea watanzania na hasa humu JF ya matumizi ya neno wife material je hivi hatuona kama tunawadhalilisha wanawake au dada zetu?

Kivipi?

Nimejaribu kutafuta tafsiri ya neno material kwa kiswahili nikapata neno Nyenzo, sikuishia hapo nikaenda mbele zaidi ya kutafuta maana rahisi ya neno nyenzo nikapata kuwa ni vifàa au kifaa cha kufanyia shughuli fulani au mashine rahisi.

Kwa tafsiri hizo na nyingine nyingi ndio maana nikafikia muktadha wa kusema kwamba kuna maneno mengine tumezoea kuyatumia lakini tunaposha.

Karibuni.
 
sina imani kwamba kila neno la kingereza lina tafsiri ya moja kwa moja kwa ivyo unavyo dadavua wewe,

mfano ni transiletie sentesi " mimi sio mtu wa mchezo mchezo " in english!
 
Kwani wife material anatakiwa awe na sifa gani?
 
Siyo maneno yote yanaweza kufanyiwa tafsiri halafu yakawa na maana inayoeleweka. Lakini nimekuelewa unamaanisha nini. Nadhani neno "kupata jiko" ndiyo linaweza kuwa na huo udhalilishaji ulioutaja.
 
Reactions: BRN
Je wanaume kibamia hawadhaliliki ?
Mbwai mbwai tuu[emoji1][emoji2][emoji1]
 
tatizo lako wewe ni kilaz.a hujui kiingereza.
 
Reactions: BRN
Hujui Kiingereza wala Kiswahili. Nani kakwambia Material tafsiri yake kwa mukhtadha huu ni Nyenzo? Kwa kukusaidia tu ukifanya Direct Translation lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili utakosea sana, kuna neno moja lina maana tofauti kulingana na lilipotumika.

Mfano sentensi hii 'its my turn maana yake ni zamu yangu na si kona yangu au left turn maana yake ni kona ya kushoto na si zamu ya kushoto.
 
Umefanya tafsiri sisisi, kwa namna inavyotumika hapo ilitakiwa utafsiri maana yake kwa kuzingatia muktadha wa neno lilivyotumika.
 
ahsante mkuu naheshimu mawazo yako, ila mkosoaji mzuri ni yule anayekuja na majibu ya kile kilichokosewa.
 
Boss kama utaendelea kutumia tafsiri sisisi ktk kila muktadha utaumia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…