Ijue Kamati Maalum ya maridhiano kuhusu uchaguzi Mkuu uliofutwa Zanzibar

Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,812
1,824
wahusika
1. Dr. Shein, chairman (incumbent president) -CCM

2. Maalim Seif (1st vice president)-CUF

3. Balozi Seif Ali Iddi (2nd vice president)-CCM

4. Mzee Ali Hassan Mwinyi (retired Zanzibar and Tanzania president)-CCM

5. Dr. Karume (retired Zanzibar president)-CCM

6. Dr. Salmin Amour, komandoo (retired Zanzibar president)-CCM

5 CCM against 1 CUF

Iko wapi check and balance hapo?

==========================

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumamosi 26 Desemba, 2015 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mazungumzo hayo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema lengo la Mazungumzo hayo ilikuwa ni kumpa taarifa Rais Magufuli juu ya hali ya mazungumzo ya kisiasa yanayoendelea huko Tanzania Zanzibar baada ya uchaguzi Mkuu.

Rais Shein amesema mazungumzo juu ya hali ya Zanzibar yanaendelea chini ya Kamati Maalum ambayo yeye ndiye Mwenyekiti na wengine wakiwa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungo wa Tanzania Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume na Rais Mstaafu wa awamu ya tano wa Zanzibar Dkt. Salmin Amour.

Amesema tayari kamati hiyo imeanza mazungumzo tangu tarehe 09 Novemba, 2015 na kwamba mazungumzo hayo yamelenga kujadili hatma ya Zanzibar baada ya uchaguzi Mkuu.

Rais Shein amebainisha kuwa mazungumzo hayo bado yanaendelea.

"Kwa hiyo nimekuja kumpa taarifa Mheshimiwa Rais Magufuli kuhusu maendeleo ya Mazungumzo yetu ili aweze kujua kinachoendelea akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo Zanzibar ni sehemu yake, na sisi ni jukumu letu kumpa taarifa hiyo" Alisema Rais Shein.

Aidha Rais Shein ameongeza kuwa Mazungumzo hayo yatakapokamilika wananchi watajulishwa.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

26 Desemba, 2015
 
Sefu ni msanii tu,mnapoteza bure muda wenu kumtetea.kitendo tu cha kujichukulia sheria mkononi na kujitangazia matokeo kinyume cha sheria ya zanzibar,hapo ndipo alipoteleza
 
Sefu ni msanii tu,mnapoteza bure muda wenu kumtetea.kitendo tu cha kujichukulia sheria mkononi na kujitangazia matokeo kinyume cha sheria ya zanzibar,hapo ndipo alipoteleza
Mimi alinifurahisha sana kuweza kuzuia wabaka demokrasia kushindwa kumtangaza "mshindi" wao. Ni historia mpya imeandikwa Tanzania. Kwa mara ya kwanza tokea uchaguzi mkuu unaoshirikisha vyama vingi. Moja ya Tume za uchaguzi Tanzania imeshindwa kumtangaza mgombea wa chama dola kuwa ni mshindi wa nafasi ya urais.

Wala haihataji elimu kujua kuwa CCM iliangukia pua.

Tayari inajulikana tokea 1995 CCM imekuwa inabaka demokrasia huko Zanzibar. Ubakaji huu wa demokrasia ni jipu sugu ambalo mtumbua majipu linamweka katika nafasi ya kuwa shujaa wa demokrasia au kushirikiana na vibaka wa demokrasia na kuukumbatia unafiki na maigizo ya uchaguzi Tanzania.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, mimi ni msema kweli na nauchukia unafiki.
 
Ili wamtait akubaliane na yao (mpango siri/matakwa )hata kama akikabidhiwa rungu atafanya ya hao mabosi wapya sio waliomtuma!
 
Sefu ni msanii tu,mnapoteza bure muda wenu kumtetea.kitendo tu cha kujichukulia sheria mkononi na kujitangazia matokeo kinyume cha sheria ya zanzibar,hapo ndipo alipoteleza
Wewe gamba usiwe biased...........
Mbona Makamba Junior naye alifanya hivyo hivyo?
Aliitisha kikao cha waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa Magufuli ndiye Rais wa awamu ya 5 kwa mujibu wa matokeo waliyokusanya wao CCM na alifanya hivyo kabla ya NEC haijatangaza rasmi matokeo ya jumla ya Urais.
Mbona uchaguzi wa huku Bara nao haukufutwa kama ilivyotokea huko Zenji?
Kitu kinachotokea Zanzibar ndiyo kile kitu alichoeleza yule mama kwenye BMK kule Dodoma mwaka jana kuwa Zanzibar haiwezi kamwe kuja kutolewa kwa vijikaratasi vya kupigia kura!
 
Ndio maana hata wazanzibari cuf wenyewe wanaonekana kupotezea.
 
Kwani watapiga kura?
Wapige kura gani tena wakati kura zilishapigwa tarehe 25/10/2015 na Mwenyekiti wa ZEC akawa keshatangaza matokeo ya majimbo 31 na washindi wote wa Baraza la Wawakilishi wakiwa tayari weshakabidhiwa vyeti vyao vya ushindi na Fomu zote za matokeo zikiwa zimasainiwa na mawakala wote wa vyama vya siasa wakiwemo na wa CCM na CUF??
Lakini kwa mshangao mkubwa Jecha akakurupuka na kuufuta uchaguzi huo bila hata ya kushirikisha Makamishna wenzie wa ZEC katika uamuzi wake huo wa kuibaka demokrasia.
Jambo lililoshangaza zaidi ni kuwa mara tu baada ya kutangaza tangazo lake hilo 'batili' wale 'waliomuamrisha' kufanya hivyo wakampeleka mahali kusikojulikana kujificha ambapo hajawahi tena kuonekana hadharani hadi leo!
 
nina wasiwasi sana na maalim seif. nimeanza kupoteza imani naye sana.....
Lakini Mkuu kumbuka hiyo ndiyo kamati ambayo imekuwa ikikutana mfululizo kwa zaidi ya mara 8 sasa tokea yule jamaa anayeitwa Jecha kuamua kuibaka demokrasia kwa lengo la kuwaokoa jamaa zake wa magamba na 'dhahama' ya kushindwa uchaguzi.
 
Mimi alinifurahisha sana kuweza kuzuia wabaka demokrasia kushindwa kumtangaza "mshindi" wao. Ni historia mpya imeandikwa Tanzania. Kwa mara ya kwanza tokea uchaguzi mkuu unaoshirikisha vyama vingi. Moja ya Tume za uchaguzi Tanzania imeshindwa kumtangaza mgombea wa chama dola kuwa ni mshindi wa nafasi ya urais.

Wala haihataji elimu kujua kuwa CCM iliangukia pua.

Tayari inajulikana tokea 1995 CCM imekuwa inabaka demokrasia huko Zanzibar. Ubakaji huu wa demokrasia ni jipu sugu ambalo mtumbua majipu linamweka katika nafasi ya kuwa shujaa wa demokrasia au kushirikiana na vibaka wa demokrasia na kuukumbatia unafiki na maigizo ya uchaguzi Tanzania.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, mimi ni msema kweli na nauchukia unafiki.
Naweza kudiriki kumuita Maalim Seif kama shujaa wa karne hii kwa kuwa kitendo cha kujitangaza mshindi wa kiti cha Urais wakati akiwa tayari keshakusanya matokeo yote ya vituo vya huko Zenji, ilikuwa surprise kubwa kwa magamba na iliharibu kabisa 'move' ya maccm ya adhma yao waliyoizoea huko Zenji ya kumtangaza mshindi wa kiti cha Urais ambaye hakushinda kwenye sanduku la kura..........
 
Back
Top Bottom