Mkuuu tunasubiiri gharama zake
Samahani kwa kuchelewa kuweka gharama hapa, Ni kutokana Na pilika za maisha, sasa nipo tayari, nataka nitumie lugha Na hesabu nyepesi kabisa Ili nipate kueleweka.....
Tuchukulie may be Sebure yako Ina ukubwa wa 120 square foot, ambapo Ni ukubwa wa wastani wa sebure nyingi, Materials cost itakua wastani wa 500,000
huku gharama za ufundi zikiwa wastani wa 700,000.
Hivyo ndo tuseme gharama zote kwa 1 Square foot Ni sawa Na 10,000.....kama ukubwa wa kazi yako unazidi Square foot 300 labda 500 ama 1,000 pia ntakupunguzia Na gharama kwa maana itakua chini ya 10,000 kwa square foot.
Kama sehemu yako inahitaji michoro tunaita broadcasting basi itategemea Na mchoro unaotaka, Kama Ni logo ya kampuni, hotel ama media house Na unataka ionekane kwenye floor pale mtu anapoingia Tu ndani, hivyo vyote Ni makubaliano, ama Ni michoro flani unataka ionekane kwenye floor za Lounge ama Night club au hata Sebureni vyote Ni kuelewana coz inategemea Na mchoro ama painting style unataka...
siwezi kumchora Mungu Tu vile sijawahi muona otherwise chochote unachotaka tunakifanya kwenye floor! Naimani mtakua mmepata picha, karibuni kwa maswali!