Ijue Club 27: Club ya wanamuziki maarufu wanaokufa wakiwa na umri wa miaka 27

Last emperor

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
10,352
9,810
Nawasalimia wakuu wangu,

Baada ya kuangalia Documentary ya Kurt Cobain inayoitwa Montage of Heck (2015), nimeshawishika kuandika kuhusu Club 27, ambayo inawakilisha namba ya wasanii maarufu 34 ambao walikufa katika umri mdogo wa miaka 27 kwasababu mbalimbali. Sababu kubwa ya vifo vyao vinatokana na matumizi makubwa ya madawa ya kulevya,pombe na hata kujiua ili wawemo katika hii club ya watu maarufu.

Mtu anaweza kufa katika umri wowote, lakini kufa kwa wanamuziki wengi maarufu,nguli na matajiri katika umri huu wa miaka 27 umefanya watu wengi kudadisi sababu hasa inayowafanya watu 'watake kufa' au wafe katika umri huu. Wenyewe wameanza hata kutunga nyimbo na kuimba Live fast Die young.Wengi wamekuwa wakihusisha na imani za kishetani,hasa ukizingatia wanamuziki wengi kati ya hawa wanatokea katika aina ya muziki wa Rock n Roll,ambao ni maarufu kwa kutukuza mambo ya kumwabudu shetani.

Wanamuziki waliokufa katika umri huu ni wengi,lakini mimi nitapenda kuwaongelea wachache watakaowakilisha wengine kwasababu vyanzo vya vifo vyao vinafanana.Miongoni mwa wanamuziki maarufu waliopo katika Club hii 27 ni;

i) Brian Jones- Huyu ni mwanamuziki mwanzilishi wa kundi la Rolling Stone, kundi linalopiga muziki wa Rock, miongoni mwa mwanamuziki maarufu anaepatikana katika kundi hili ni Mick Jagger. Mwanamuziki huyu Brian Jones aliishi mwaka 1942-1969, na alikutwa amekufa katika nyumba yake kwenye bwawa la kuogelea akiwa anaelea baada ya kujiover dozi na madawa ya kulevya.

ii) Jimmy Hendrix - Huyu ni mwanamuziki mweusi ambae inasemekana ndio mcharazaji bora wa electric guitar wa muda wote..Pia ni mwimbaji maarufu wa muziki wa Rock n Roll.Aliishi kuanzia mwaka 1942-1970, huyu ni mwanamuziki ambae alitoa quotation maarufu inayosema "When the power of LOVE,overcome the love of POWER,the world will know peace".Alikufa akiwa na miaka 27 kwa kinachosadikiwa na kuzidiwa na matumizi ya madawa ya kulevya na pombe.

iii) Amy Winehouse - Ni mwanamuziki wa kike alieishi kuanzia mwaka 1983-2011,alikuwa akiimba muziki wa Soul, na Rhythm and Blues.Huyu amekufa juzijuzi tu na watu wengi humu kama ni wafuatiliaji wa muziki kama hawajasikia nyimbo zake wamelisikia jina lake..Alikuwa maarufu sana katika umri mdogo tu,na akiwa na umri wa miaka 24 tu alikuwa ameshachukua tuzo za grammy 6! Alikufa kwa over doze ya pombe na madawa ya kulevya.

iv) Kurt Cobain - Huyu ni mwanamuziki na pia alikuwa kiongozi wa kundi la muziki la Nirvana. Aliishi kuanzia mwaka 1967-1994.Alijiua kwa kujipiga risasi kichwani kwa kutumia shortgun. Kifo cha Kurt Cobain ndicho kilisababisha dunia nzima kujiuliza kuna nini hasa nyuma ya hiyo watu kujiua wakiwa na miaka 27 ili tu wawe katika Club 27? Mama yake na Kurt Cobain akiongea na gazeti la Daily World alisema "Now he is gone and joined that stupid club,I told him not to join that stupid club", Yaani ameenda kujinga na hiyo club yao ya kijinga,nilimbwambia asijiunge na hiyo club ya kijinga. Hii inaonyesha kuwa Kurt alijiua makusudi ili ajiunge na hiyo Club 27.Swali ni je kuna nini nyuma ya kufa ukiwa na miaka 27 mpaka kupelekea mpaka wengine wajiue ili wawemo tu kwenye Club 27?

230px-Amy_Winehouse_f4962007_crop.jpg

Amy Winehouse

jimi-hendrix.jpg

Jimi Hendrix
 
Nimesikia pia hiyo club yaani ulijiunga huko hautakiwi ufike 28 yrs kwenye hii dunia.
But unakuwa maarufu faster sana na bata LA nguvu but 27 yrs ndio mwisho wako.
But nadhani hizi ni kamba za cult za kishetani hao wanamuziki wanakuwa hawajui kinachoendelea but wao wanakuwa kama SADAKA kwa hizo cult za kishetani.
Ni sawa na ile utajiri wa mbeya wa KUKU kidonoa punje za mahindi akila 7 utaishi miaka 7 ya utajiri the u die.
So it's just a stupid CLUB nadhani ni branch tu za illuminat
 
Nimesikia pia hiyo club yaani ulijiunga huko hautakiwi ufike 28 yrs kwenye hii dunia.
But unakuwa maarufu faster sana na bata LA nguvu but 27 yrs ndio mwisho wako.
But nadhani hizi ni kamba za cult za kishetani hao wanamuziki wanakuwa hawajui kinachoendelea but wao wanakuwa kama SADAKA kwa hizo cult za kishetani.
Ni sawa na ile utajiri wa mbeya wa KUKU kidonoa punje za mahindi akila 7 utaishi miaka 7 ya utajiri the u die.
So it's just a stupid CLUB nadhani ni branch tu za illuminat
Kweli mkuu..ni sawa na ile ya Mbeya ya vipunje.Na wanakuwa maarufu kweli kweli
 
jimmy hendrix alikuwa noma sana, alikuwa left handed si unaona gitaa ameligeuza juu chini? Rhythms zinazotoka hapo ni hatariiii...alifia uingereza nadhani
 
Back
Top Bottom