Igunga, Tabora: Jela miaka 20 kwa kumvua nguo

Igunga, Tabora: Jela miaka 20 kwa kumvua nguo

Vipi mkuu, umewahi kuzaa au kuzalishwa?
Nna watoto 6.Sema hilo siyo kosa la kumfunga mtu miaka 20,.Usichukulie ghazabu,kwani baada ya kumshika alimfanya nini?kuna watu wa kuwafunga hiyo miaka 20 lakini mahakama zenu zinawaachia huru au kuwafunga kifungo kidogo tu.
 
MAHAKAMA ya Hakimu Wilaya ya Igunga mkoani Tabora imemuhukumu kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela, Mtandi Nassoro (24) mkazi wa Igunga baada ya kupatikana na hatia ya shambulio la aibu kwa mtoto mwenye umri wa miaka mitano (jina limehifadhiwa).

Mwendesha Mashtaka wa Polisi Elimajidi Kweyamba alidai kwamba mshtakiwa Mtandi alimfanyia kosa la shambulio la aibu mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitano Mei 18, mwaka huu saa nne asubuhi katika Mtaa wa Stoo mjini Igunga.

Kweyamba alidai Nassoro alimvua nguo za ndani na kisha kumshika shika kwenye sehemu zake za siri mtoto huyo.

Mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo aliposomewa shtaka lake mahakamani mapema mwaka huu na ndipo upande wa Jamuhuri ulipopeleka mashahidi watano, akiwamo mtoto aliyeshambuliwa.

Wote walitoa ushahidi na kumtambua mshtakiwa huyo.

Hakimu Milanzi alisema kwamba baada ya mahakama hiyo kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, iliridhishwa bila kuacha shaka yeyote kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamuhuri umemtia hatiani mshtakiwa Nassoro.

Alimhukumu adhabu ya kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka 20, ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia hiyo.
Akirudi.big g.tsh 7000.mwendoka Kasi utakua dar to mwanza via tabora.
 
Nna watoto 6.Sema hilo siyo kosa la kumfunga mtu miaka 20,.Usichukulie ghazabu,kwani baada ya kumshika alimfanya nini?kuna watu wa kuwafunga hiyo miaka 20 lakini mahakama zenu zinawaachia huru au kuwafunga kifungo kidogo tu.
Kwa hiyo kwako wewe kosa la kuiba bilioni 30 na kumshika Mtoto mdogo uchi wake lipi lina uzito mkubwa?
 
Back
Top Bottom