Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 754
- 3,097
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imemuhukumu adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kijana wa miaka 20, kwa kosa la kubaka mtoto wa kaka yake wa miaka 14.
Elius Mgashi mkaazi wa Mtaa wa Stoo mjini Igunga, amepewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji.
Mwendesha Mashitaka kutoka Jeshi la Polisi wilaya ya Igunga Elimajid Kweyamba, alidai kwamba katika tarehe tafauti kati ya Septemba 14 na 19 mwaka 2018 katika mtaa wa Stoo mjini Igunga, mshitakiwa huyo alifanya mapenzi na mtoto wa kaka yake ambaye ana umri wa miaka 14.
Mbele ya Hakimu wa wilaya ya Igunga Lydia Ilunda, Kweyamba aliifahamisha mahakama kwamba, kutenda hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 130 (1) (2) (e) na 131 (1) vya kanuni ya adhabu sura ya 16, mapitio ya mwaka 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo.
Hata hivyo, baada ya mshitakiwa kusomewa shitaka hilo alikana, ndipo upande wa Jamhuri ulipeleka mahakamani mashahidi watano akiwemo mhanga wa tukio hilo, ambao wote walimtambua mshitakiwa.
Mahakama hiyo baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, Hakimu Lydia Ilunda alisema, pasi na shaka ushahidi uliotolewa mahakamani na upande wa Jamhuri imemuona mshitakiwa Elius Mgashi ana hatia.
Akitoa hukumu ya shauri hilo, Hakimu Lyidia Ilunda alisema kuwa, mahakama inamuhukumu Elius Mgashi kutumikia adhabu ya kifungo cha jumla ya miaka 30 jela, ili iwe fundisho kwa vijana wengine wanaobaka wasichana wadogo na kuwaharibia maisha yao